Powered By Blogger

Wednesday, September 26, 2012

SIMBA, YANGA ZAINGIA MAFICHONI

 Wachezaji wa Simba wakiwasili Zanzibar
 Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kikiwasili Zanzibar
 Kikosi cha Yanga
 Simba hao
Kwa raha zao

WAKONGWE wa soka nchini, Simba na Yanga, zimelikimbia jiji la Dar es Salaam na kwenda kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo umepangwa kucheza Septemba 3 mwaka huu, katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, itamenyana na Yanga ambayo ni mabingwa wa kombe la Afrika Mashariki na Kati.

Wekundu wa msimbazi tayari wamepiga kambi Zanzibar kwa ajili ya mchezo huo wa kukata na shoka huku Yanga wakidaiwa kujificha katika mji wa Bagamoyo.

Simba hadi sasa inaongoza ligi hiyo kwa kufikisha poti tisa kibindoni baada ya kushinda michezo yao mitatu waliyoicheza katika uwanja wa Taifa na kuwa na magoli saba.

Nao Yanga hadi sasa wamejikusanyia pointi nne baada ya kushinda mchezo mmoja na kusuluhu mmoja huku ikipoteza mchezo mmoja.