Fatma Ali
Huyo ni Shomari Zizu akifanya majambozi
Mtoto Pori, Mohammed Alli kama kawaida
Mwasiti Kitoronto naye yumo
Hadija Yussuf akiwaambia wazibe njia sio riziki
Hapo ni kiduku mbele kwa mbele
Chezea Miriamu weeeee
Mtoto wa Mfalme, Abubakar Sudi 'Amigo' ndani ya nyumba
Malkia Leilah Rashid roho kwatuuuuuuuuuuu
Kama kawaida Mcharuko akifanya majambozi yake
Big Daddy Mzee Yussuf akinogesha akiwa na dogo Hemedi
Umeonaaaa maufundi kwenda mbele
WAKALI wa muziki wa mipasho nchini, Jahazi Morden Taarab 'Wana wa nakshinakshi' usiku wa leo watatibwirika katika ukumbi wao wa nyumbani, uliopo Travetine Hotel Dar es Salaam.
Jahazi wakiongozwa na Mkurugenzi wao, 'Big daddy' Mzee Yussuf, watajinafasi vya kutosha katika ukumbi huo.
Mzee Yussuf, amepania kutoa burudani ya kutosha katika onyesho hilo na amewaomba wapenzi wa kundi hilo kujitokeza kwa wingi.
Amesema onyesho hilo, limepangwa kuanza saa tatu usiku mpka majogoo ambapo ameahidi kutoa burudani ya kutosha.