MALKIA kwa raha zake
Kidugu kama kawa
Mfalme
Huyo ni mtoto wa Mfalme anaitwa AmigoBabu Ali akipapasa kinanda
Chidi Boy
Crew ya Jahazi
Huyo ni Miriam Amour
Mama lao Hadija Yussuf
Mauji anachana nyuzi
Mtoto Pori Mohammed Ali
Mgeni Said akicheza na Keybod
Mama Mcharuko
Kiduku mbele kwa mbele
Mussa Mipango
M ussa Baziii 'Baba warida' akikung'uta gita
Mzee Yussuf akifanya mambo yake
Mwasiti MC naye yumo
Juma Mgunda 'Jino Mmoja'
Mara kapinda mgongo mara kanyanyua mguuuuu
WAKALI wa mipasho nchini, Jahazi Morden Taarab usiku wa leo linatarajia kuachia burudani ya kufa mtu katika ukumbi wa Hotel Travetine uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam.
Jahazi wakiongozwa na Mkurugenzi wa kundi hilo, Big Daddy Mzee Yussuf, watateremsha kikosi chao kamili katika onyosho hilo maalumu kwa ajili ya wakazi wa Magomeni na Vitongoji vyake.
Mzee Yussuf 'Mfalme' alisema onyesho hilo litakuwa la aina yake kwani watapata fursa ya kupiga nyimbo zao mpya zitakazokuwa katika albamu ya 9.
Mfalme aliwaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi katika onyesho hilo maridadi ambapo ameongeza kuwa wataimba nyimbo zote zinazotamba na zilizowahi kutamba kwenye anga za muziki.