Powered By Blogger

Friday, September 14, 2012

MFALME MZEE YUSSUF KUKAMUA CANADA

 Viduku kwenda mbele
 Wazee wa vidukuuuu
 Malkia  kama kawaida
 Fatrna Mcharuko akiwa kazini
 Mama wa maruperupe
 Mcharuko kama kawa
 Chezea Amigo wee
 Amigo, Anaringanaringa mpenzi.
 Utanibeba leo, umekunywa soda zangu
 Big Dady akiwarambisha mashabiki wake
 Zungu la Unga, Musa Bezi, akipiga mpini
 Mauji mauji, Mauji anachana nyuzi..........

WAKALI wa muziki wa mipasho, Jahazi usiku wa leo itatibirika na mashabiki wake katika ukumbi wa Mashujaa uliopo Vingunguti Dar es Salaam.

Onyesho hilo litaanza saa tatu usiku mpka majogoo na Jahazi itashuka na waimbaji wake wote katika onyesho hilo.

Mkurugenzi wa kundi hilo, 'Big daddy' Mzee Yussuf, alisema watatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zao mpya zitakazokuwa katika albamu yao ya 9 itakayozinduliwa mwisho mwa mwaka.

Alisema albamu hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali kutoka na nyimbo zake kusheheni vina na mizani huku waimbaji mahiri wakishirikishwa kwenye albamu hiyo.

Katika hatua nyingine Mzee Yussuf, alisema mwezi unaokuja anatarajia kufanya onyesho la aina yake nchini Canada.

Onyesho hilo, litafanyika kufuatia mwaliko kutoka kwa wapenzi wa kundi hilo lenye mashabiki kila kona ya dunia.

Big daddy, alisema baada ya onyesho hilo ambalo atalifanya kwa siku mbili atawasili nchini kuendelea na maonyesho mengine ya kila siku.

Amewaomba wapenzi na mashabiki wa kundi hilo kuendelea kushirikiana na kundi hilo ili wapate burudani ya kutosha.