Powered By Blogger

Sunday, September 30, 2012

SIMBA YAENDELEA KUNG'ARA LIGI KUU

 MRISHO NGASA AKISHANGILIA BAO LA PILI
 WACHEZAJI WA SIMBA WAKISHEREHEKEA
 MWENYEKITI WA SIMBA, ISMAIL ADEN RAGE AKITIBWIRIKA NA MASHABIKI WA TIMU HIYO
 AMIRI MAFTAHA AKITAFAKARI BAADA YA KULIMWA RED CARD
NGASA AKIJARIBU KUWATOKA WACHEZAJI WA PRISON

 WEKUNDU wa Msambazi ama Simba ya Dar es Salaam imeendeleza wimbi lake la ubingwa baada ya kuwapigisha kwata maafande wa Prison kutoka Mbeya.

Mchezo huo uliokuwa wa kasi na kuvutia, Prison walikuwa wa mwanzo kuliona lango la Simba katika dakika ya saba ya mchezo baada ya mshambuliaji wake Elias Maguri kuweka mpira kimiani.

Kuingia kwa bao hilo, kuliasha hasira za Mnyama huyo wa pori anayesadikiwa kuwa mwenye nguvu nyingi kuliko Mnyama yoyote na ndipo dakika ya 45  Felix Sunzu aliwainua mashabiki wa Simba baada ya kuipatia timu yake bao la kusawazisha.

Kipindi cha pili kiklianza kwa kasi ambapo Simba ilionekana kuliandama lango la Prison kama mithili ya nyuki aliyepigwa ndimu katika nyumba yake yalimfanya Mrisho Ngasa kuipatia timu yake bao la pili.

Hata hivyo, Wekundu hao wa Msimbazi weanaojiandaa kukabiliana na watani zao Yanga walipata pigo baada ya beki wao mahiri Amiri Maftaha kulimwa kadi nyekundu kutokana na mchezo mchafu.