Powered By Blogger

Monday, September 24, 2012

NJOO JAHAZI UKUTANE NA WAIMBAJI HAWA

 Ukutane na Mzee Yssuf
 Fatma Ali
 Fatma Mahamoud Mcharuko
 Big Daddy
 Utamuona Mohamed Ali
 Chidi Boy utamuona live
 Fatma Ali kila siku yupo
 Utakutana na waimbaji wote hao
 Fatma Ali
 Pia, utawaona hawa kila mmoja anavyonogesha
 Mtoto pori hakosi
 Mashabiki waliofurika kila siku
 Dada na Kaka utakutana nao bila zengwe
 Hata Malkia utamuona
 Kikosi hichi chote kipo
 Amigo anavyomwagiwa mafedha naye utakutananaye
 Chidi na Babu Ali utaona mamabo yao
 Waimbaji hawa utawakuta tu
 Leila na marafiki zake utawaona wakiserebuka
Miriamu Amour naye utamkuta


WAKALI wa mipasho nchini, Jahazi wiend hii, itawasafirisha wapenzi na mashabiki wake walioko katika visiwa vya karafuu mjini Zanzibar.

Jahazi itawasili Zanzibar Ijumaa hii ambapo itafanya onyesho la kukata na shoka.

Mkurugenzi wa Jahazi Mzee Yussuf 'Big Daddy' alisema onyesho hilo litakuwa mahususi kwa mashabiki wao wa visiwani.

Alisema katika onyesho hilo, ambalo litakuwa la aina yake, wataanza kuimba nyimbo zao mpya ukiwemo wa wasiwasi wako ndio maradhi yake ambao utabeba jina la albamu.

Alisema Jumamosi bendi hiyo itarejea Dar es Salaam kuendelea na maonyesho mengine.