'Big Daddy' Mfalme Mzee Yussuf
Mfalme katika pozi
Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf
Hapa ni Amigo akitamba na Fullshangwe
Malkia Leilah Rashidi
Huyu ni Miriamu Amour akitamba na 'Penye neema hapakosi fitna'
WAKALI wa muziki wa mipasho nchini, Jahazi usiku wa leo umepania kutoa burudani ya kukata na shoka katika ukumbi wa Moshi Bar, Kipunguni, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kundi hilo mahiri, 'Big Daddy' Mzee Yussuf, amesema show hiyo itakuwa maalumu kwa wakazi wa maeneo hayo na vitongoji vyake.
Alisema kundi hilo, litashuka na waimbaji wake wote mahiri akiwemo yeye mwenyewe, Malkia Leilah Rashid, Fatma Ali, Miriamu Amour, Hadija Yussuf, Fatma Mahamoud 'Mcharuko', Mwasiti Kitoronto.
Nyoto wengine watakaohudhuria onyesho hilo ni Amigo, Mohamed Alli, Mud Maugo, Mussa Bass, Babu Ali, Chidi Boy, Tall, Mwanne Athuman 'Mama lao', Mgeni Saidi na wengine wengi.
Amesema katika onyesho hilo Jahazi itapiga nyimbo zake zote mpya ukiwemo wa Mpenzi Chokleti, Zibeni njia sio riziki, Sina mda huo, Full shangwe, na zote zinazotamba na zilizowahi kutamba.
Amewaomba wapenzi na mashabiki wa kundi hilo kujitokeza kwa wingi katika onyesho hilo, ili waweze kupata burudani ya kutosha.