Hasani Moshi, Edo Sanga na Juma Katundu
Haya twendeeee
Wazee wa Msondo wakiwa kazini.Dede na Mzee Ngulumo
Hapa ni Hamis Mnyupe na Romarioo wakipuuliza tarumbeta.
WAKONGWE wa muziki wa dansi hapa nchini, Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' leo watakonga nyoyo za
mashabiki wao katika ukumbi wa Max Bar Ilala.
Onyesho hilo limepangwa kuanza saa 12 jioni mpaka saa sita usiku, ambapo Msondo imepanga kufanya kweli katika onyesho hilo.
Wanamuziki wa bendi hiyo kongwe wakiongozwa na Muhidini Ngurumo, Said Mabela, Romario, Dede, Juma Katundu, Hasani Moshi na wengine wengi.