Amigo kama kawaida
Chidi boy akipapasa kinanda
'Big daddy' na dada yake Hadija
Fatma Mcharuko akinogesha
Hawa ni Hadija na Asma Machupa akiwa katika vazi la kimasai
Waimbaji wa Jahazi wakiwajibika
Chezea Hadija weeeeeeeeeeeeeeee
Kiroho safi, kama umbeya wewe tuuuuuuu
Kiduku usipime
Malkia Leila Rashid naye yumoooo
Nogesha baba nogeshaaa
Malkia akijinafi
Sina mda huoooooooooo
Mtoto pori ndani ya nyumba
Mussa baziii, piga gitaaa
Mgeni Said akinogesha mambo
Mashabiki wakijimwaya mwaya
Mfalme Mzee Yussuf akitoa burudani
Utanibeba leo umekunywa soda yanguuuuuuu
RATIBA YA JAHAZI WIKI HII
WAKALI wa mipasho nchini, Jahazi leo wanatarajia kuachia burudani ya kukata na shoka katika ukumbi wa Koyanga Kiwalani, kesho bendi hiyo chini ya Mzee Yussuf atawapagawisha mashabiki wa Manyara Park Tandale na Ijumaa itafanya onyesho lake katika ukumbi wa Mashujaa Vingunguti.
Jahazi imepania kutoa burudani ya aina yake katika ukumbi wa Rufita Tabata Jumamosi ijayo. Maonyesho hayo yataanza saa 3 usiku mpka majogoo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa bendi hiyo, Mfalme Mzee Yussuf, waimbaji wote wa Jahazi watakuwepo kwenye maonyesho hayo na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Alisema katika maonyesho hayo, Jahazi watapiga baadhi ya nyimbo zao zilizomo kwenye albamu ya 9 itakayozinduliwa mapema mwaka huu.