Umuone Mfalme Mzee Yussuf
Malkia Leila Rashid
Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf
Utamuona Fatma Mahamudu Mcharuko
Amigo atakuwepo
Mohamed Ali utakutananaye
Amigo atakuonyesha mambo yake
Mcharuko kama kawaida yake atawapagawisha
Hadija na Mauji utawaona kama walivyo
Mashabiki kama hawa watakuepo
Utamuona Leila anavyoikata bia
Hata hawa unaweza kuwaona
Mzee Yussuf anavyotunzwa fedha utamkuta
Mashabiki wastarabu kama hawa utawaona
Kikosi cha manahodha wa Jahazi kitakuepo chote hicho
Hassani anavyomwagia mapesa bosi wake
JAHAZI leo litawasafirisha wapenzi na mashabiki wake wanaoishi mitaa ya Yombo na Vitongoji vyake katika ukumbi wa Gadafi Square Yombo.
Safari ya Jahazi itaanza kutiananga katika viunga hivyo kuanzia saa tatu usiku chini ya nahodha wake Big Daddy Mzee Yussuf.
Jahazi ambalo kwa sasa ndio linalopakiza mashabiki wengi litasafiri na waimbaji wake wote wenye uzoefu wa kuimba na upigaji wa ala tofauti.
Onyesho hilo litatumiwa na Jahazi kuzitangaza nyimbo zake mpya zitakazokuwemo kwenye alabamu ya tisa ya bendi hiyo mahiri hapa nchini.