Mshambuliaji wa Yanga akichuana na beki ya Lyon
Mashabiki wa Yanga
Kikosi cha Yanga
Sunday, September 30, 2012
jAHAZI, KHADIJA KOPA, CHID BENZI KUPAGAWISHA TARAVETINE USIKU HUU
Mzee Yussuf 'Mfalme'
Khadija Kopa
Malkia Khadija Kopa
Chid Benz
Mtoto Pori Mohamed Ali
Fatma Ali
Chezea Chidi Boy weee
Miriam Amour
Mama Mcharuko
Kirikuu 'Amigo'
Hadija na Mauji
Mussa Bezi huyoo
Mgeni Said
Mussa Mipango
Big Daddy Mzee Yussuf
WAKALI wa muziki wa mipasho, Jahazi jioni hii wanatarajia kufanya onyesho la aina yake katika ukumbi wa Travetine Hotel Magomeni, Dar es Salaam.
Onyesho hilo limedhaminiwa na Dida Clasic litaanza saa tatu usiku mpaka majogoo na litawashirikisha wasanii kibao wakali.
Miongoni mwa wasanii watakaosindikiza onyesho hilo ni pamoja na mkali wa mipasho nchini Khadija Omari Kopa, Chid Benzi na wengine kibao.
Kiingilio katika onyesho hilo kimepangwa kuwa sh. 7000 na tiketi zitapatikana mlangoni.
Mzee Yussuf amepania kufanya mambo makubwa katika onyesho hilo akiwa pamoja na waimbaji wenzake
Khadija Kopa
Malkia Khadija Kopa
Chid Benz
Chid
Leilah RashidMtoto Pori Mohamed Ali
Fatma Ali
Chezea Chidi Boy weee
Miriam Amour
Mama Mcharuko
Kirikuu 'Amigo'
Hadija na Mauji
Waimbaji wa Jahazi
Babu Ali akipapasa kinandaMussa Bezi huyoo
Mgeni Said
Mussa Mipango
Big Daddy Mzee Yussuf
WAKALI wa muziki wa mipasho, Jahazi jioni hii wanatarajia kufanya onyesho la aina yake katika ukumbi wa Travetine Hotel Magomeni, Dar es Salaam.
Onyesho hilo limedhaminiwa na Dida Clasic litaanza saa tatu usiku mpaka majogoo na litawashirikisha wasanii kibao wakali.
Miongoni mwa wasanii watakaosindikiza onyesho hilo ni pamoja na mkali wa mipasho nchini Khadija Omari Kopa, Chid Benzi na wengine kibao.
Kiingilio katika onyesho hilo kimepangwa kuwa sh. 7000 na tiketi zitapatikana mlangoni.
Mzee Yussuf amepania kufanya mambo makubwa katika onyesho hilo akiwa pamoja na waimbaji wenzake
SIMBA YAENDELEA KUNG'ARA LIGI KUU
MRISHO NGASA AKISHANGILIA BAO LA PILI
WACHEZAJI WA SIMBA WAKISHEREHEKEA
MWENYEKITI WA SIMBA, ISMAIL ADEN RAGE AKITIBWIRIKA NA MASHABIKI WA TIMU HIYO
AMIRI MAFTAHA AKITAFAKARI BAADA YA KULIMWA RED CARD

NGASA AKIJARIBU KUWATOKA WACHEZAJI WA PRISON
WEKUNDU wa Msambazi ama Simba ya Dar es Salaam imeendeleza wimbi lake la ubingwa baada ya kuwapigisha kwata maafande wa Prison kutoka Mbeya.
Mchezo huo uliokuwa wa kasi na kuvutia, Prison walikuwa wa mwanzo kuliona lango la Simba katika dakika ya saba ya mchezo baada ya mshambuliaji wake Elias Maguri kuweka mpira kimiani.
Kuingia kwa bao hilo, kuliasha hasira za Mnyama huyo wa pori anayesadikiwa kuwa mwenye nguvu nyingi kuliko Mnyama yoyote na ndipo dakika ya 45 Felix Sunzu aliwainua mashabiki wa Simba baada ya kuipatia timu yake bao la kusawazisha.
Kipindi cha pili kiklianza kwa kasi ambapo Simba ilionekana kuliandama lango la Prison kama mithili ya nyuki aliyepigwa ndimu katika nyumba yake yalimfanya Mrisho Ngasa kuipatia timu yake bao la pili.
Hata hivyo, Wekundu hao wa Msimbazi weanaojiandaa kukabiliana na watani zao Yanga walipata pigo baada ya beki wao mahiri Amiri Maftaha kulimwa kadi nyekundu kutokana na mchezo mchafu.

YAFAHAMU MAISHA YA ROMARIO KIMZIKI
ROMAN MNG'ANDE 'ROMARIO'
Mng'ande, ni msanii mwenye historia kubwa na aliyejipatia umaarufu mkubwa katika historia ya muziki wa nchi hii.
Umaarufu wa msanii huyo, haukuja hivi hivi bali ulitokana na mambo mbalimbali ikiwemo vituko na vichekesho vingi anavyofanya akiwa kwenye kazi yake hiyo.
Msanii huyo, amekuwa masikioni mwa mashabiki wengi hususan wapenzi wa muziki wa dansi kutokana na mbwembwe zake.
Akizungumza juzi, Mng'ande, anaanza kuizungumzia historia yake kimuziki ambapo anasema alianza kujiingiza kwenye bahari hiyo mwaka 1973 akiwa katika kundi la Father Kanuti, mkoani Morogoro.
Anasema akiwa kwenye kundi hilo, alianza kwa kupiga vyombo mbalimbali ikiwemo tarumbeta ambalo anauzoefu nalo mkubwa.
Mng'ande, anasema katika kundi hilo, alidumu kwa miaka sita ambapo mwaka 1979 alijiunga na kundi la Urafiki Jazz lililokuwa na masikani yake jijini Dar es Salaam.
Anasema kilichomsukuma kujiunga na kundi la Urafiki kipindi hicho ni kukuza kipaji chake cha muziki na kujipatia ukomavu.
Mng'ande, ambaye anasifika kwa vituko na tambo za kila aina, anasema katika kundi hilo hakuweza kudumu kwa muda mrefu kutokana na kuhitajika katika kundi la Tanzania Stars Magosi.
Anasema mara kwa mara viongozi wa bendi hiyo, walikuwa wakimfuata ili aweze kujiunga nalo na kuiongezea nguvu bendi hiyo.
Msanii huyo, anasema mwaka 1981 uongozi wa Tanzania Stars Magosi, ulifanikiwa kumuhamisha katika bendi ya Urafiki, baada ya kumpandia dau.
"Unajua sisi wasanii ni kama vile wachezaji mpira mtu akikupandia dau huwezi kuliacha lazima umfuate...tunafanya mziki ili tupate hela sasa kama umepewa hela utaweza kuziacha.
"Ndio maana hata nilipofuatwa na viongozi wa Tanzania Magosi sikuweza kukataa kwani niliangalia maslahi mbele mambo mengine badae," anasema.
Anasema mwaka 1983, alidumu katika bendi hiyo na alifanikiwa kujiongezea umaarufu na kuanza kusikika masikioni mwa mashabiki wengi.
Mng'ande ambaye ni baba wa watoto wanne, anasema hata hivyo, hakuweza kudumu kwa muda mrefu katika bendi hiyo na akaanza kufuatwa na viongozi wa Juwata Jazz kipindi hicho sasa Msondo Ngoma.
"Kama unavyojua nyota njema huonekana asubuhi na ndivyo ilivyoanza kungara kwangu...historia yangu ya muziki ni ndefu lakini inaonyesha jinsi nilivyoanza kufanikiwa," anasema.
Anasema baada ya kufuatwa na viongozi wa Juwata na kuonyesha nia ya kutaka kumchukua kwenye kundi hilo, hakufanya kosa na aliwaambia milango iko wazi.
"Lengo langu lilikuwa kuimba kwenye bendi kubwa kama Juwata, hivyo nilipofuatwa sikufanya kosa nikawaambia milango iko wazi waje tuzungumze.
"Kwa kweli viongozi wale hawakusita walinifuata na kunieleza dhamira yao ni kutaka nijiunge na bendi ile ambayo kipindi hicho ilikuwa moto wa kuotea mbalimbali," anasema.
Anasema mwaka 1983, alijiunga rasmi na bendi ya Juwata Jazz, wakati huo ikiwa na waimbaji mahiri akiwemo marehemu TX Moshi William, Said Mabera na wengine wengi.
Mng'ande, anasema tokea kipindo hicho hadi sasa hajatoka kwenye bendi hiyo wala hafikirii kutoka mpaka atakapoamua kuachana na muziki.
"Kama nilirogwa basi viongozi wa Juwata walipata mganga kwani tokea nilipojiunga na bendi hiyo hadi sasa sijatoka wala sifikirii kutoka hata iweje.
"Nimepata mafanikio makubwa nikiwa katika bendi hiyo na imenisaidia kufahamiana na watu wengi, viongozi wa serikali, kwa kweli nimepata mafanikio makubwa katika maisha yangu.
"Siwezi kusita kuwa bendi ya Msondo, imenitoa kimaisha, imenifanya kiwango changu cha muzimki kukua siku hadi siku, siwezi kuisahau katika maisha yangu yote," anasema.
Anasema baada ya kupata mafanikio mengi katika bendi hiyo, anafikiria kujenga maisha yake ili aweze kuishi vizuri na familia yake.
Mng'ande, anasema hana mpango wa kuanzisha bendi na lengo lake ni kuzidi kujiimarisha katika kazi yake hiyo ili bendi yake iweze kufanya vyema.
Anasema katika maisha yake ya muziki hawezi kumsahau marehemu TX Moshi kwani alikuwa rafiki yake mkubwa na alikuwa akimshauri mambo mengi.
Romario, anasema waimbaji wengine ambao hawezi kuwasahau ni pamoja na Said Mabera na Muhidini Ngurumo.
Anasema wimbo ambao hawezi kuusahau ni kibao cha 'Isikutonza iyudi chaum' uliotungwa na marehemu Mwanjiro na alishiriki kwa kiasi kikubwa kupiga vyombo katika wimbo huo.
"Huu wimbo ukipigwa hata niwe wapi lazima ni simame kidogo niusikilize, naupenda sana kuliko wimbo mwingine, nilishirikishwa kuupiga," anajigamba.
Msanii huyo ambaye amesoma katika shule ya sekondari Kingurunyembe, Morogoro anasema albamu za Msondo ambazo hawezi kuzisahau ni pamoja na Mwanaume tumeumbwa mateso, Kilio cha mtu mzima.
Romario mbali na kipaji cha kupuliza tarumbgeta lakini amejaaliwa kipaji cha uimbaji ambapo mara nyingi ameonekana akiimba nyimbo mbalimbali.
AMIGO: KICHWA KIMOJA VIPAJI MIA MOJA,
Abubakari Sudi 'Amigo'
IFAHAMU HISTORIA YAKE.
KUNA msemo unasema wizi wa maendeleo ni ule wa kuiga ndio maana ukitaka kufanikiwa katika maisha ni lazima uige namna watu wanavyoishi ndio uanze maisha.
Nimekumbuka msemo huo baada ya kukutana na muimbaji anayechipukia kwa kasi katika kundi la Jahazi Morden Taraab, Abubakar Sudi 'Amigo' na kisha kuanza kunisimulia historia ya maisha yake.
Amigo ama wengi wanamfahamu kwa jina la mtoto wa Mfalme anasema kilichomsukuma kuingia kwenye muziki ni kuvutiwa na muimbaji mahiri wa dansi Mwinjuma Muumini 'Kocha wa dunia'.
Anasema "Nyimbo zake za Tunda na Kilio cha yatima, nilikuwa nikizihusudu sana na kila nilipokuwa nazisikia nilitamani siku moja niwe kama yeye," ndivyo alivyanza mazungumzo yake Abubakari Sudi 'Amigo'.
Amigo ambaye hivi sasa amekuwa midomoni mwa mashabiki wengi hususan wa muziki wa taarab kutokana na umahiri wake wa uimbaji.
Miongoni mwa mambo yanayosababisha mashabiki wamkubali muimbaji huyo anayeimbia kundi la Jahazi Morden Taarab ni baada ya kuachia wimbo unaoitwa Full shangwe ambao umekuwa gunzo la jiji hivi sasa.
Akizungumza na Jarida la Jiliwaze mwishoni mwa wiki, Amigo alisema alijiunga na Jahazi mwishoni mwa mwaka 2009 akitokea katika kundi la East Afrika Melody 'Watoto wa mjini'.
Alisema baada ya kuingia mkataba na Jahazi chini ya Mkiurugenzi wake, Mfalme Mzee Yussuf, alipewa wimbo unaoitwa Domo kaya.
Amigo, ambaye mara nyingi mashabiki wanamuitwa 'Mtoto wa Mfalme' anasema wimbo huo ulianza kumpatia umaarufu mkubwa.
Alisema baada ya kuonekana kufanya vizuri katika wimbo huo uliokuwa kwenye albamu ya Daktari wa Mapenzi, ndipo Yussuf alipohamasika kumpatia wimbo wa Full shangwe ambao hivi sasa umekuwa gumzo la jiji.
Amigo, anakiri kwamba wimbo wa Full shangwe umemfanya awe midomoni mwa mashabiki wengi wa taarab hivi sasa na daima atamshukuru Yussuf kwa kumtungia kibao hicho.
"Katika hili sina budi nimshukuru sana Mzee Yussuf kwa kunifanya nifike hapa nilipo, baada ya kunitungia wimbo wa Full shangwe umeniongezea umaarufu mkubwa.
"Kupitia kwa Mzee kumenifanya ningara kimaisha na kimuziki, ni mtu ambaye amejaaliwa roho ya pekee yake na Mungu tofauti na viongozi wengine wa bendi wenye roho za kwanini," alisema.
Alisema kwa sasa hana mpango wa kulihama kundi la Jahazi na kwamba anachokifanya ni kuongeza juhudi ili aweze kufikia lengo alililojiwekea kimuziki.
Muimbaji huyo mwenye umbo dogo, alisema lengo lake ni kuvaa viatu vya Yussuf ili awe muimbaji bora, mtungaji na mpigaji.
Alisema ushirikiano uliopo baina ya waimbaji wa Jahazi na viongozi wa kundi hilo ndio uliomfanya awe juu kimuziki.
Muimbaji huyo alisema kabla hajajiingiza kwenye muziki alikuwa akimuhusudu sana Mwinjuma Muumini 'Kocha wav duniani' na ndie aliyesababisha ajiingize kwenye muziki.
HISTORIA YAKE KATIKA MUZIKI.
Amigo, alisema alianza rasmi kujiingiza kwenye muziki mwishoni mwa mwaka 2004.
Alisema kipindi hicho alianzia kwenye kundi la muziki wa kizazi kipya lililofahamika kama Karama's Camp na akiwa katika kundi hilo alibahatika kuimba nyimbo mbili ambazo ni Sina mwengine na Nimefanyaje.
Kwa mujibu wa muimbaji huyo, kundi la Karama's Camp lilianzisha kundi lingine la Segere ambapo alikuwa akiimba nyimbo tofauti tofauti.
Alisema baada ya mudi kundi hilo lilipanuka na kuanzisha lingine lililofahamika kama East rusha roho.
Muimbaji huyo, alisema mwaka 2008 alijiunga na kundi la East Afrika Melody, ambapo alibahatika kuimba wimbo unaoitwa Ilove U, ambapo mwishoni mwa 2009 alijiunga na Jahazi.
MATARAJIO YAKE.
Amigo, alisema anatarajia kucheza filamu ambapo hivi sasa tayari ameshatayarisha filamu inayofahamika kama Ladha ya Maharage.
Alisema filamu hiyo imewashirikisha wakongwe wa filamu hapa nchini akiwemo Dk. Cheni, Sebe, Riami na wengine wengi. Amigo, alisema filamu hiyo iko jikoni na inatarajiwa kupakuliwa muda wowote kutoka sasa.
Alisema kipaji cha uigizaji anacho muda mrefu na alishawahi kupata mafunzo kwa ajili ya kuendeleza kipaji hicho.
Amigo, alisema pamoja na kuimba taarab hivi sasa lakini anatarajia kuimba muziki wa kizazi kipya kuendeleza kipaji chake.
Alimazilizia mazungumzo yake kwa kusema, alimaliza darasa la saba katika shule ya Msingi Makumbusho mwaka 1999 na mwaka 2000-2003 alimaliza kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Al-haramaini, zote za Dar es Salaam.

Friday, September 28, 2012
JAHAZI KUTIBWIRIKA ZANZIBAR
Big Daddy
Fatma Ali
Waimbaji wa Jahazi
'Baba Kirikuu' Amigo
Mohamed Ali
Fatma Mcharuko
Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf
Babu Ali
Malkia Leila Rashid
Mfalme Mzee Yussuf
Mussa Bezi
Director Mohamed Mauji
Miriamu Amour
Mgeni Said
Mussa Mipango
Jahazi ikiongozwa na Mzee Yussuf tayari imeshawasili katika visiwa hivyo kwa ajili ya onyesho hilo kabambe ambalo wapenzi na mashabiki wa Zanzibar watapata fursa ya kujionea mashamumshamu kutoka kwa magwiji hao wa mipasho.
Fatma Ali
Waimbaji wa Jahazi
'Baba Kirikuu' Amigo
Mohamed Ali
Fatma Mcharuko
Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf
Babu Ali
Malkia Leila Rashid
Mfalme Mzee Yussuf
Mussa Bezi
Director Mohamed Mauji
Miriamu Amour
Mgeni Said
Mussa Mipango
WAKALI wa mipasho Jahazi Morden Taarab, usiku huu wataporomosha burudani ya aina yake katika visiwa vya marashi ya karafuu pale Zanzibar.
Thursday, September 27, 2012
MFAHAMU SHARO MILIONEA
Sharo katika pozi
UNAPOZUNGUMZIA tathinia ya filamu hapa nchini huwezi kulisahau jina la Hussein Mkieta ambaye amekuwa midomoni mwa watu wengi kutokana na ustadi mkubwa wa kuigiza hususan vichekesho.
Mkieta kama anavyofahamika na wengi kwa jina la Sharomilionea ni kijana mtanashati ambaye nyota yake inazidi kungara siku hadi.
Katika miaka ya hivi karibuni tasnia ya maigizo hususan vichekesho imekuwa kwa kasi kubwa ba hilo limeendana sambamba na kuibuka kwa vipaji vipya katika sanaa hiyo.
Sharomilionea ni miongoni mwa wasanii wa vichekesho ambao wanazidi kujizolea umaarufu na sifa kemkem kutokana na umahiri wake wa kutoa burudani ikihusisha sanaa ya vichekesho pamoja na muziki wa kizazi kipya.
Mkiet amefanikiwa kuteka nyoyo za mashabiki na wapenzi wengi wa vichekesho kutokana na umahiri huo ambao hivi sasa anazidi kuteka soko la sanaa hapa nchini.
Msanii huyo ambaye mashabiki wake wengi ni vijana na watoto pamoja na wazee amekuwa akibuni staili mbalimbali kuvutia mashabiki wake hususdan kwa kutia madoido ya Kimagharibi na kujiweka katika maisha ya juu katika uigizaji wake.
“Niliamua kuwa mbunifu ili kutafuta staili tofauti na wachekeshaji wengine na ninashukuru hilo limeweza kufanikiwa na sidhani kama kuna mtu anaweza kunifikia kwa sasa," anasema mchekeshaji huyo.
Msanii huyo ambaye amekuwa akishirikiana bega kwa bega na mchekeshaji maarufu hapa nchini Amri Athuman 'King Majuto' anaweka wazi kwamba ingawa anapenda kuigiza maisha ya juu binafsi hapendi kuishi maisha ya aina hiyo.
"Niko tofauti sana na vile jamii inavyoniona kupitia maigizo yangu...huwa sipendi kuishi maisha kama yale ila pale nipo kazini ndio maana ninaonekana vile," anasema.
Anasema lengo lake la kuigiza staili ya aina ile ni kuwafundisha wenye tabia kama hizo kuacha kwani binadamu wote ni sawa na hakuna aliyebora kuliko mwingine.
Mkiet anasema kuna baadhi ya watu katika jamii wanapokuwa na maisha tofauti na watu wengine hupenda kujionyesha na kuwadharau wenzao ambao maisha yao ni yakawaida na kwamba jambo hilohalipendi katika maisha yake.
“Binafsi siishi maisha yale na wala siyapendi kabisa maana nawaonyesha ili waweze kuachana na tabia hizo kwa kuwa hazina maana yoyote zaidi ya kuonyesha ni jinsi gani walivyokuwa malimbukeni kuiga maisha ya watu wa Magharibi”anasema.
Kwa mujibu wa Mchekeshaji huyo, anakiri kwamba asingeweza kufikia hapo alipo sasa bila ya kumsahau Mzee Majuto ambaye amemfundisha mambo mengi ya sanaa.
Anasema Mzee Majuto amemsaidia kwa kiasi kikubwa kufikia hapo alipo na kamwe hawezi kusahau mchango wake katika tathinia ya sanaa hapa nchini.
"Ninawashukuru wasanii wenzangu wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamenipa msaada mkubwa hadi kufikia hapa nilipo...Mzee Majuto ni jembe langu ambalo siwezi kulisahau katika maisha yangu yote ," anasema.
Mkiet licha ya kujikita katika sanaa ya vichekesho lakini anajihusisha na muziki wa kizazi kipya ambapo pia ameonyesha kiwango cha hali ya juu kutokana na staili ya uimbaji wake.
Miongoni mwa nyimbo alizoziachia hewani msanii huyo ni pamoja na Sondela na Hawataki alioshirikiana na Rich Mavoko pamoja na Kanali Top zimefanikiwa kumuweka katika nafasi nzuri katika chati za muziki.
Anasema aliamua kujikita katika muziki kwa ajili ya kujitafutia riziki na si vyenginevyo na kuongeza kuwa hakuingia kwenye muziki kupahatisha bali amedhamiria kufanya kweli kwenye tathinia hiyo.
Historia ya mchekeshaji huyo, inaonyesha alianza kujikita katika sanaa tangu akiwa shule ya msingi Tanga na alipomaliza alifanikiwa kuja Dar es Salaam na hapo kipaji chake kilizidi kukua na kujipatia umaarufu baada ya kukutana na muigizaji mkongwe Mzee Majuto na kujiingiza moja kwa moja katika Vituko Show.
Baadhi ya filamu alizoshiriki mchekeshaji huyo kwa kushirikiana na Mzee Majuto na wasanii wengine ni pamoja na Chuma Ulete, Pedeshee, Vyumba vimejaa na Kozi Man.

ASEMAVYO JOKHA KASIMU
GWIJI WA MIPASHO JOKHA KASIMU
"KUPIGANA vijembe katika taarab hakukuanza leo wa jana, tokea enzi za marehemu Leila Khatib na Khadija Kopa walikuwa wanapigana vijembe.
"Sisi waimbaji chipukizi tumerithi kutoka kwao...siwezi kushangaa kusikia mtu anampiga vijembe mwenzake kupitia tasnia hii," anasema Jokha Kassim, muimbaji mahiri wa taarab anayeimbia kundi la Tanzania Moto.
Anasema amelazimika kulizungumzia hilo, abaada ya kuwepo tetesi kuwa muimbaji huyo mwenye sauti ya kuvutia kuwa nyimbo zake nyingi zimekuwa zikimlenga kiongozi wa Jahazi, Mzee Yussuf na mke wake Leila Rashid.
Jokha, ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Yussuf na kubahatika kupata mtoto mmoja anayeitwa Yussuf, tangu walipoachana kumekuwa na minong'ono kuwa muimbaji huyo amekuwa akiimba nyimbo za mafumbo na kumpiga vijembe mtalaka wake huyo.
Akizungumza hivi karibuni, Jokha anaanza kwa kusema muziki ni malumbano na mambo ya kujibizana kupitia fani hiyo imeanza zamani.
Anasema anakumbuka tangu akiwa mdogo, waimbaji walikuwa wakijibizana kupitia tasnia hiyo na haoni ajabu sasa waimbaji kuendelea kujibizana kupitia muziki.
"Nakumbuka marehemu Leila Khatibu na Khadija Kopa walivyokuwa wakipigana vijimbe wala lengo lao halikuwa baya ilikuwa ni kuvuta mashabiki.
Hata hivyo, muimbaji huyo, anasema si kweli kama nyimbo zake anazoimba zinalenga kuwapiga vijembe Yussuf na Leila na kwamba anafikisha ujumbe kwa jamii husika.
Anasema majibizano kwenye muziki ni vitu vya kawaida na hashangazwi waimbaji kujibizana kwani kunaleta changamoto nyingi.
Jokha, anayetamba na kibao cha domo la udaku, alioutoa hivi karibuni anasema hakumlenga mtu katika wimbo huo.
Anasema mpangilio wa mashairi yanayopatikana kwenye wimbo huo, yamekuwa yakileta tafsiri mbaya kwenye jamii ambao wengi wanadhani alimlenga mtu.
Jokha, anasema wimbo huo haukumlenga mtu yoyote bali ulingela kuielimisha jamii mambo mbalimbali yanayotokea.
Anasema hivi sasa anajiandaa kuachia kibao chengine anachoamini kuwa kutakuwa moto wa kuotea mbali.
Akizungumzia maisha yake ya muziki hivi sasa tangu alipojiunga na kundi la T. Motto, anasema mambo yanakwenda vizuri na kipaji chake kinazidi kukua.
Anasema akiwa katika kundi hilo, wamebahatika kurikodi albamu inayoitwa 'Aliyeniumba hajanikosea' ambayo ilikuwa gunzo la jiji.
Jokha, anasema hivi sasa wako mbioni kupakua albamu mbili kwa mpigo, ambazo ni Mimi staa na Domo la udaku.
Anasema baadhi ya nyimbo katika albamu hizo zimekamilika na amezitaja kuwa ni pamoja na mwanamke hashuo, domo la udaku, mimi staa na wewe si daktari wa mapenzi.
Jokha, anasema wako katika hatua za mwisho kwa ajili ya uzinduzi wa albamu hizo na tayari baadhi ya nyimbo hizo wameshaanza kuwasikilizisha mashabiki wao.
Anamalizia kwa kuwaomba wapenzi na mashabiki wake wake mkao wa kula kuzipokea albamu hizo na anawaomba mashabiki wake wategeme mambo mazuri kutoka kwake.

TAMASHA LA MUZIKI, HAPATOSHI LEADERS
ISHA MASHAUZI
JIKE LA SIMBA ISHA MASHAUZI
WANENGUAJI WA BENDI YA MASHUJAA
WACHEZA SHOO WA MASHUJAA
RAPA WA FM ACADEMIA, NYOSI AL-SADATI
NYOSI-AL SADAT AKIWA NA BENI KINYAIA KATIKATI
WAIMBAJI WA MSONDO NGOMA WAKIONGOZWA NA MUHIDIN NGURUMO

WAPULIZA TARUMBETA WA MSONDO
TAMASHA kubwa la muziki wa dansi nchini ambalo loitashirikisha bendi mbalimbali maarufu litafanyika leo katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
Bendi hizo ni pamoja na Msondo Ngoma 'Baba ya muziki', Fm Academia, Mashujaa Band, Mashauzi Classic, DDC Mlimani Park 'Sikinde' na nyingine nyingi.
Maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na lengo lake ni kukisaidia Chama cha muziki wa dansi Tanzania (CHAMUDATA).
Katika tamasha hilo, kiingilio kitakuwa ni sh. 20,000 viti maalumu, sh. 5,000 viti vya kawaida na kwamba bendi ya Isha Mashauzi na Khadija Kopa zitasindikiza.
Subscribe to:
Posts (Atom)