Umuone Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf
Ukutane na Big Daddy Mzee Yussuf
Uonane na Mussa Bezi
Kikosi hicho kitakuepo
Hata dada na kaka utawaona hivi hivi
Mcharuko atawapagawisha mashabiki wake
Mauji akichana nyuzi zake
Mashabiki watulivu kama hawa utakutananao
Amigo hakosi abadani
Hata Malkia Leila Rashid atatia timu
Shosti Fatma Ali utakutananaye
Kama hujawahi kumuona Mgeni Said leo utamuona
Bibie Miriamu Amour atakuepo
Mtoto Pori ndani ya nyumba
Utamuona Mwasiti Kitorontro
Mussa Mipango
Wakali wa mipasho hapa nchini Jahazi usiku huu watakonga nyoyo za mashabiki wao katika ukumbi wa Travetine hoteli Magomeni.
Onyesho hilo ikiwa ni mfululizo wa shangwe za sikukuu ya eid el hajj zitaanza kurindima majira ya saa tatu usiku mpka majogoo.
Kiongozi wa Jahazi 'Big Daddy' Mzee Yussuf atakuwa nahodha katika onyesho hilo na atawaongoza waimbaji wote wa kundi hilo mahiri hapa nchini.