Powered By Blogger

Saturday, October 27, 2012

MNYAMA ALAMBA KONI ZA AZAMU

 LEBO YA SIMBA
 WACHEZAJI WA SIMBA WAKIFURAHIA MOJA YA GOLI LAO
 HATOKI MTU HAPA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba jana iliziyeyusha koni za Azam baada ya kuinga timu hiyo kwa 3-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Azamu ilikuwa ya mwanzo kupata goli baada ya mshabuliaji wake mahiri John Boko 'Adebayo' kuiadikia timu hiyo bao la kwanza.

Hata hivyo, Simba ilizinduka na kulishambulia lango la Azamu kama nyuki na ndipo mshambuliaji hatari wa Simba aliyetokea Azam, Mrisho Ngasa aliposawazisha goli hilo.

Emmanuel Okwi alizidisha machungu langoni mwa Azamu baada ya kupachika magoli mawili na hadi kipenga kinamalizika Simba tatu na Azamu moja.

Kwa matokeo hayo Simba iko kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 23 na kuwaacha nyumba mahasimu wao Yanga wakiwa na pointi 20 huku Azamu wakishika nafasi ya tatu.

Nao Yanga walifanikiwa kuharibu gwaride la JKT Olijoro baada ya kuwafunga goli moja kwa buyu katika mchezo uliopigwa mjini Arusha.

Bao la Yanga lilifungwa na Mbuyu Twite na hadi mwisho wa mchezo Yanga ilitoka uwanjani kifua mbele dhidi ya timu hiyo.