Big Daddy
'MUACHE Mfalme aitwe Mfalme' mara nyingi mashabiki wa burudani hususan taarab wamekuwa wakisikika wakisema hivyo kutokana na kukunwa vilivyo na muimbaji na mtunzi mahiri wa nyimbo za taarab
(mipasho) hapa nchini Big Daddy Mzee Yussuf.
Mzee Yussuf ambaye ni kiongozi wa Jahazi Morden Taarab hivi sasa unaweza kusema hakamatiki kutokana na kujipatia umaarufu kila kona ya dunia.
Kutokana na kipaji na uwezo mkubwa aliojaaliwa na Mungu, mashabiki wa Mzee Yussuf wanaoishi nchini Canada wamempa mwaliko wa siku kama nne hivi kwenda kutoa burudani katika mijiji ya nchi hiyo.
Mzee Yussuf, aliondoka usiku wa Alhamis iliyopita na tayari hivi sasa ameshafanya maonyesho kadhaa nchi humo ambapo yameonekana kutia fora na kuwagusa wazungu kinomanoma.
Akizungumza na akiwa Canada Big Daddy alisema ameshukuru kupata mapokezi makubwa na tayari ameshafanya show kwenye kumbi tofauti ambapo ameacha gunzo kubwa kwa wapenzi na mashabiki wake.
'Big Daddy' Mzee Yussuf alisema ziara hiyo ni kutokana na kufanya vizuri kwenye masuala ya burudani ndani na nje ya nchi kupitia muziki wa taarab.