Huyo ni Mohamed Ali
Mama Mcharuko kama kawaida yake
Bibie Fatma Ali
Malkia wa mipasho Hadija Kopa aliimba na Chid Benzi
Big Daddy Mzee Yussuf akirapu na Chid Benzi katika onyesho hilo
ICON wa muziki wa taaraba hapa nchini Mfalme Mzee Yussuf usiku wa kuamkia leo aliwaacha hoi mashabiki wake baada ya kuimba wimbo wa bongo fleva alioshirikishwa na Chid Benzi.
Kutokana na wimbo huo, mashabiki lukuki waliojitokeza katika onyesho hilo walimwagia sifa kiongozi huyo wa Jahazi na kumuona tofauti na waimbaji wengine wa taarab.
Baada ya kupanda jukwaani kwa Mzee Yussuf mashabiki walionekana kumpa sapoti kubwa huku wakimshangilia muda wote aliokuwa akirapu.
Hali hiyo ilisababisha mashabiki kupiga mayowe ya furaha huku wakimwagia fedha na sifa kemkem kutokana na umahiri wake.