WAKALI wa muziki wa taarab hapa nchini Jahazi Morden Taarab kesho wamepania kufanya shoo kambe katika ukumbi wa Travetine Hoteli.
Kiongozi wa kundi hilo Mzee Yussuf alisema onyesho hilo litakuwa la aina kutokana na kundi hilo kujipanga kikamilifu kwa ajili ya kutoa burudani siku hiyo.
Aliwaomba wapenzi na mashabiki wao kujitokeza kwa wingi katika onyesho hilo.