Powered By Blogger

Wednesday, July 27, 2011

Hao wa wale wakali wa nyimbo za taarab hapa nchini na nje ya nchi. Ni kundi zima la Jahazi linaloongozwa na Mfalme Mzee Yussuf. limepania kufanya onyesho maalumu siku ya Jumamosi wiki hii katika ukumbi Travetine Hoteli Magomeni. Onyesho hilo litasindikizwa na Wela wela, Baikoko kutoka Tanga, na kitu Tigo.
Siku hiyo Jahazi itapiga nyimbo zake zote mpya pamoja na zile zinazotamba na zile zilizowahi kutamba.
Kiingilio katika onyesho hilo itakuwa sh. 7000. Mzee Yussuf amepania kufanya mambo makubwa siku hiyo. Nyote mnakaribisha katika shoo hiyo ya vunja jungu.