Powered By Blogger

Thursday, July 28, 2011

HAYAWI HAYAWI sasa yamefika. ile siku inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi na mashabiki wa bendi ya Jahazi Morden Taarab (Wana wa nakshinakshi), ndio inakaribia ambapo Jumamosi wiki hii itafanya kweli katika ukumbi wa hoteli Travetine pale Magomeni.

Show hiyo maalumu kwa ajili ya vunja jungu itapambwa na kundi la Baikoko kutoka Tanga, Kitu Tigo na kitu Kimba vyote vya Jijini Dar es Salaam, kiingilio katika onyesho hilo ni sh. 7000 tu.

Mzee Yussuf ameahidi kufanya kweli siku hiyo kwa kuimba vibao vyake vyote vinavyotamba na vilivyowahi kutamba. Munaombwa kuhudhuria kwa wingi katika onyesho hilo la aina yake.