Wakali wa muziki wa taarab hapa nchini bendi ya Jahazi leo wameanza ziara ya wiki moja kwenye mikoa ya Kusini pande za Lindi na Mtwara. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa bendi hiyo, Mzee Yussuf kundi hilo usiku wa leo litafanya onyesho lake pale Rufiji ambapo wapenzi na mashabiki wataramba vitu adimu kutoka Jahazi.
Mzee anayetamba na wimbo wa 'wagombanao ndio wapatanao' aliomshirikisha dada yake Hadija Yussuf alisema katika ziara hiyo Jahazi imeambatana na waimbaji wake wote mahiri na watapiga nyimbo zao zote mpya.
Alisema ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya wakazi wa mikoa hiyo na amewaomba kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya kundi hilo lililosheheni viapaji kibao.
Mzee Yussuf alisema kundi hilo linatarajia kurudi mkoa Dar es Salaam, na litapiga shoo yake ya mwisho hapa Dar siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Travetine Hoteli, Magomeni. amewataka wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Mungu awajaalie safari njema na murudi salama.
Imeandikwa na mtayarishaji wa Blog hii, Mudy Tela aka. Mzee wa London.