Malkia Leilah Rashid akiwa jukwaani
'Big Daddy' Mzee Yussuf akiweka pozi mbele ya duka lake lililopo Kariakoo
Hapa ni Miriamu Amouri akiimba na mashabiki wake
Mtoto wa Mfalme, Amigo akiwaimbisha mashabiki wake kibao chake cha Full Shangwe
Huyu ni sauti ya Chiriku Hadija Yussuf, akiwajibika jukwaani
WAKALI wa muziki wa taarab nchini, Jahazi Morden, wanatarajia kuachia burudani ya aina yake katika onyesho litakalofanyika Jumapili hii ukumbi wa Travetine Hoteli Magomeni, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kundi hilo, na muimbaji mahiri Mzee Yussuf 'Big Daddy' alisema onyesho hilo litatumika kutambuilisha baadhi ya nyimbo zao mpya zitakazokuwemo katika albamu yao ya tisa.
Alisema albamu hiyo itazinduliwa mwishoni mwa mwaka huu, na kwamba mashabiki wataanza kuzisikiliza nyimbo hizo kwenye maonyesho mbalimbali ili waweze kuzifahamu.
Mfalme alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo sita na itaandaliwa katika ubora wa hali ya juu ili mashabiki waweze kupata ladha tofauti tofauti.
Aliwaomba mashabiki na wapenzi wa kundi hilo kujitokeza kwa wingi katika onyesho la Jumapili ili kuweza kuzisikia nyimbo hizo.
Kundi la Jahazi kwa sasa linatamba na albamu yake ya Mpenzi Chokleti, yenye nyimbo sita ambazo zimejizolea umaarufu mkubwa masikioni mwa mashabiki wa muziki wa mipasho nchini.