Mtoto wa Mflame, Abubakari Sudi Amigo, akikonga nyoyo za mashabiki wake
Miriamu Amour, akijinafasi kwa raha zake
Malkia Leilah Rashidi, akiwaburudisha mashabiki.
Sauti ya Chiriku, Hadija Yussuf, akifanya mambo yake.
Babu Ally, akipapasa kinanda kwa raha zake.
'Big Daddy' Mzee Yussuf akiweka mambo sawa.
'Zungu la unga' Mussa Bass, akipiga gitta.
Nogesha mama nogesha.
Big Daddy akitoa burudani.
Waimbaji wa Jahazi wakiwa kazini.
Mgeni Saidi akipapasa kinanda kwa umahiri mkubwa.
STORI NA ABDALLA MENSA.
KUNDI la mipasho la Jahazi Modern Taarab, kesho linatarajiwa
kutambulisha baadhi ya rapu zao mpya, kwenye tamasha maalum lililopewa jina la ‘Usiku wa Sina Muda Huo’, litalofanyika kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Jahazi Mzee Yussuf ‘Big Daddy’ alisema, rapu hizo ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya albamu yao ya tisa, wanayotarajia kuifyatua baadaye mwaka huu, ikiwa imekusanya vibao sita alivyodai kuwa, vyote ni moto wa kuoteambali.
Yussuf ambaye ni kati ya watunzi, waimbaji na wapapasaji mahiri wa kinanda hapa nchini, alizitaja baadhi ya rapu hizo zilizoko kwenye mtindo unaochezeka, kuwa ni pamoja na ‘Yamemnogea’, ‘Kukopi na Kupesti’, ‘Kelele Zimekwisha’ na ‘Wanapatana’.
“Wapenzi pamoja na mashabiki wetu wote watakaopata bahati ya
kuhudhuria tamasha hilo, watapata fursa ya kufaidi uhondo wa rapu hizo ambazo naamini kuwa, zitafunika nyingine zote zilizotangulia, kutokana na kwamba ziko kiubunifu zaidi,” alisema.
Alisema, mbali ya rapu hizo, tamasha hilo limepangwa kuanza saa 3:30 usiku litanogeshwa na shoo ya kukata na shoka
kutoka kwa kikundi chao cha kiduku kiitwacho ‘Jahazi Kiduku Dancers’.
Miongoni mwa nyimbo zinazotamba katika kundi hilo na waimbaji wake kwenye mabano ni pamoja na Mpenzi Choleti (Mzee Yussuf), Sina Mda Huo (Leilah Rashid), Zibeni Njia sio ridhiki (Hadija Yussuf), Full Shangwe (Abubakar Sudi) na Mtaniona hivihivi (Fatma Mahamudu).