Malkia Leilah Rashid akitoa Burudani.
Akijinafasi kwa raha zake.
Hapa Fatma Alli akifanya majamboziiiii...
Akikonga nyoyo za mashabiki wake.
Chezea Fatma weeeee.
Mtoto Pori ndani ya nyumba.
Mohamme Alli, akipeana mikono na mashabiki wake.
Kanyaga kanyaga kanyaga...bong'oa bong'oa.
Waimbaji wa Jahazi wakiwa stejini.
Hapa wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali.
'Big Daddy' akifanya mambo yake.
sauti ya Chiriku Hadija Yussuf akipagawisha mashabiki wake.
NA MWANDISHI WETU.
WAKALI wa mipasho nchini, Jahazi Morden Taarab usiku wa kuamkia leo wamewaacha hoi mashabiki wao baada ya kuwaporomoshea burudani ya jkukata na shoka katika ukumbi wa Travetine Hotel, Magomeni.
Jahazi, wakiongozwa na Mkurugenzi wao, 'Big Daddy' Mzee Yussuf, aliziteka vya kutosha nyoyo za maelfu ya mashabiki waliohudhuria onyesho hilo maalumu.
Onyesho hilo lilikuwa la kwanza baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kufanyika katika ukumbi huo.
Waimbaji wa bendi hiyo, yenye mashabiki wengi kuliko zingine hapa nchini, waliongozwa na Mfalme, Malkia Leilah Rashidi, Hadija Yussuf, Miriamu Amour, Fatma Alli, Abubakari Sudi 'Amigo', Fatma Mahamudu 'Mcharuko'.
Waimbaji wengine waliopamba jukwa katika onyesho hilo, ni Fatma Machupa, Mohammed Alli 'Mtoto Pori', Kidawa, Mwasiti Kitoronto, Mwasiti Mbwana 'MC', Mwanne.
Huku wapapasa kinanda waliongozwa na Chidi Boy, Babu Alli, Tall. Upande wa gita waliongozwa na Director Mudi Maugo, Mussa Bass, Juma Mgunda, Mussa Mussa.