Hapa ni 'Big Daddy' Mzee Yussuf akiwapa raha mashabiki wake
Kama kawaida, akiimba kibao cha Mpenzi Chokleti.
Kanyaga kanyaga komoa komoaaaaa.
Mfalme akiwa na mcheza kidugu wake Hemedi wakifanya mambo
Mpaka chini ni kiduku kwenda mbeleeee tu.
Haya chukue namba yangu. Mzee Yussuf akibadilishana namba na mashabiki wake
Asane tutakupigia mkuu, mashabiki wakimshukuru Mfalme baada ya kuwapa namba yake ya simu.
NA MWANDISHI WETU.
KIONGOZI na muimbaji mashuhuru wa kundi la Jahazi Morden Taarab, Big Daddy Mzee Yussuf, yuko mbioni kutoa albamu yake binafsi hivi karibuni.
Mfalme ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kwa uimbaji na utungaji wa nyimbo za taarabu hapa nchini na nje ya nchi, amesema albamu hiyo itakuwa tishio.
Amesema albamu hiyo kwa sasa iko jikoni na baada ya muda mfupi anatarajia kuipakuwa ambapo amewaomba mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuisubiri albamu hiyo.
Big Daddy, amesema mbali na albamu hiyo binafsi kundi la Jahazi liko katika maandalizi ya mwisho kutoa albamu yake ya 9 ambapo baadhi ya nyimbo zimeshaanza kutungwa.