Hapa Mfalme akipanga CD za nyimbo mbalimbali zilizotolewa na Jahazi katika duka lake hilo
Big Daddy, akiweka pozi mbele ya duka lake.
Huyo dada hapo ni mmoja wa wauzaji wa duka hilo, akitabasamu kwa raha zake.
KIONGOZI wa Jahazi na muimbaji mahiri wa kundi hilo, 'Big Daddy' Mzee Yussuf amefungua duka lake pale mjini Kariakoo ambapo anauza vitu mbalimbali zikiwemo CD za bendi hiyo.
Duka hilo, anauza bidhaa mbalimbali ambazo ni pamoja na CD Original za nyimbo za Jahazi, kuna huduma ya DSTV, MP PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY, TTCL, DAWASCO na SASATEL.
Shop hiyo, ambayo ameiboresha vya kutosha ipo njiani kabisa imewekwa mabango mbalimbali yanayoonyesha duka lilipo kama vile MY Entetaiment.
Duka hilo lipo mkono wa kulia kama unatokea mtaa wa Magila karibu na kanisa la KKKT utakuta mbele kuna hotel ya EMMY utaingia kulia ambapo kama mita 30 utalikuta duka hilo.
Anawakaribisha wateja wote kwenda kupata huduma mbalimbali na mteja hapo ni mfalme anakaribishwa muda wote duka linafunguliwa saa 2.00 asubuhi mpaka jioni.