Powered By Blogger

Sunday, December 9, 2012

RAIS KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 51 YA UHURU WA TANGANYIKA

 Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete akiingia uwanja wa Uhuru tayari kwa maadhimisho hayo, amefuatana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange
 Gwaride likipita mbele ya Amiri Jeshi
 Amiri Jeshi, Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik akisalimiana na Rais wa Congo, Joseph Kabila
 Viongozi mbalimbali waliohudhuria
 Nia askari wa kikosi cha FFU wakipita kwa mwendo wa haraka
 Kikosi cha bendera
 Vijana wa Halaiki
 Gwaride
Rais Kikwete akikagua gadi ya askari Magereza wanawake


AMIRI Jeshi Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete aliwaongoza maelfu ya Watanzania kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika.

Sherehe hizo zilifanyika kiatika uwanja wa Uhuru, Temeke Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.

Viongozi waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mzee Mwinyi, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, Mama Maria Nyerere, Mama Fatma Nyerere, mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu, wabunge, wawakilishi, mabalozi na marais kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

Wananchi walifurika kwa wingi katika sherehe hizo ambapo uwanja wa Uhuru ulitapika na baadhi yao walilazimika kuhamia uwanja wa taifa.