'Big Daddy' Mzee Yussuf leo kuandika historia nyingine kwenye tasnia ya taarab hapa nchini kwani muda mfupi ujao atazindua albamu yake ya tisa kwenye ukumbi wa travetine hoteli Magomeni.
Uzinduzi wa albamu hiyo iliyopewa jina la Wasiwasi wako utaanza saa mbili usiku ambapo Mfalme Mzee Yussuf na kundi lake litakapoingia katika uwanja huo kwa staili ya kipekee.
Mzee Yussuf amepania kufanya maajabu katika onyesho hilo na amewaahidi wapenzi na mashabiki wake kupata ladha na vitu tofauti katika usiku wa leo.
Amesema tiketi kwa ajili ya onyesho hilo kabambe zinapatikana mlangoni na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Malkia Leila Rashid naye ataimba wimbo mpya kabisa katika albamu hiyo.
Mohammed Ali naye ataimba usiku wa leo ni wimbo mpya kabisa
Fatma Ali ataimba wimbo wake mpya
Hadija Yussuf ataimba pia
Fatma Mahamoud