Fatma Mahamuod 'Mcharuko'
Kipenzi cha mashabiki wengi Mfalme Mzee Yussuf
Umuone mtoto wa Mfalme Abubakari Sudi 'Amigo' na Full shangwe yake
Ukutane na Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf akifanya mambo yake
Mwasiti Kitoronto atakuepo
Utamuona Malkia Leila Rashid bila ya chenga
Mtoto Pori Mohammed Ali ataimba
Shosti Fatma Ali atakuepo
Ukutane na Mussa Mipango mfalme wa Bass Tanzania
Mgeni Said atakuepo
Director Mohammed Mauji
Utamuona Big Daddy Mzee Yussuf
Utakutana na Miriamu Amour
Rahma Machupa
MABINGWA wa muziki wa mipasho nchini, Jahazai usiku huu utakonga nyoyo za mashabiki wake katika ukumbi wa Taravetine Hoteli Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Jahazi wakiongozwa na Mfalme Mzee Yussuf watatia nanga katika ukumbi huo kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo.
Bendi hiyo mahiri na iliyosheheni waimbaji makini watapiga nyimbo zao mpya na zile zinazotamba kwenye anga za burudani hapa nchini.
Mkurugenzi wa Jahazi, Big Daddy Mzee Yussuf alisema onyesho hilo watatumia katika kutambulisha nyimbo zao mpya ambazo watazizindua mwishoni mwa mwezi huu katika ukumbi huo.