Powered By Blogger

Sunday, December 16, 2012

JAHAZI KUKAMU TRAVE USIKU HUU

 Big Daddy Mzee Yussuf atatoa burudanmi maridhawa leo katika ukumbi wa Travetine Hoteli ambapo Jahazi itakonga nyoyo za mashabiki wake usiku huu
 Mtoto wa Mfalme Amigo
 Malkia Leila Rashid
 Mtoto Pori Mohammed Ali
 Ni shost Miriamu Amour anayetamba na wimbo katika bendi ya Jahazi
 Unaweza kumwita Fatma Shobo muimbaji mahiri kabisa wa Jahazi
 SaUTI YA Chiriku Hadija Yussuf akiwa na Director Mohamed Mauji. Hadija anatamba na wimbo usemao Zibeni njia sio riziki
 Huyo ni Fatma Mcharuko au Mama Kijacho akimba ambapo hivi sasa anatamba na wimbo wake usemao Mtaniona hivi hivi
 Fatma Kasimu akiwa na Mfalme Mzee Yussuf. Fatma anatamba na wimbo wake Hakuna Mkamilifu
Big Daddy akiimba na mashabiki wake.

Usiku wa leo Jahazi imedhamiria kutoa burudani ya aina yake katika ukumbi wa Travetine Hoteli uliopo Magomeni Dar es Salaam.

Onyesho hilo kamambe litaanza saa tatu usiku mpaka majogoo ambapo mashabiki wa bendi hiyo mahiri wataanza kununua tiketi za uzinduzi wa albamu ya 9 wa bendi hiyo utakaofanyika Desemba 31 mwaka huu, katika ukumbi Travetine Hoteli.

Mashabiki watakaonunua tiketi leo watauziwa kwa sh. 15000 badala ya sh. 20,000 siku ya uzinduzi.

Mkurugenzi wa Jahazi Mzee Yussuf alisema wameamua kuuza tiketi hizo mapema ili kutoa fursa kwa mashabiki wao kuzipata kabla ya siku ya uzinduzi huo.