Powered By Blogger

Friday, August 31, 2012

WAIMBAJI WA JAHAZI WAKIWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI

 Hapa Mzee Yussuf akiperuzi mambo mbalimbali katika mtandao
 Malkia Leilah Rashid akiwa jukwaani
 'Big Daddy' Mzee Yussuf akiweka pozi mbele ya duka lake lililopo Kariakoo
 Hapa ni Miriamu Amouri akiimba na mashabiki wake
 Mtoto wa Mfalme, Amigo akiwaimbisha mashabiki wake kibao chake cha Full Shangwe
Huyu ni sauti ya Chiriku Hadija Yussuf, akiwajibika jukwaani

WAKALI wa muziki wa taarab nchini, Jahazi Morden, wanatarajia kuachia burudani ya aina yake katika onyesho litakalofanyika Jumapili hii ukumbi wa Travetine Hoteli Magomeni, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa kundi hilo, na muimbaji mahiri Mzee Yussuf 'Big Daddy' alisema onyesho hilo litatumika kutambuilisha baadhi ya nyimbo zao mpya zitakazokuwemo katika albamu yao ya tisa.

Alisema albamu hiyo itazinduliwa mwishoni mwa mwaka huu, na kwamba mashabiki wataanza kuzisikiliza nyimbo hizo kwenye maonyesho mbalimbali ili waweze kuzifahamu.

Mfalme alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo sita na itaandaliwa katika ubora wa hali ya juu ili mashabiki waweze kupata ladha tofauti tofauti.

Aliwaomba mashabiki na wapenzi wa kundi hilo kujitokeza kwa wingi katika onyesho la Jumapili ili kuweza kuzisikia nyimbo hizo.

Kundi la Jahazi kwa sasa linatamba na albamu yake ya Mpenzi Chokleti, yenye nyimbo sita ambazo zimejizolea umaarufu mkubwa masikioni mwa mashabiki wa muziki wa mipasho nchini.

Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Mpenzi Chokleti (Mzee Yussuf), Zibeni njia sio riziki (Hadija Yussuf), Penye neema hapakosi husda (Miriamu Amour), Full Shangwe (Abubakari Sudi Amigo), Mtaniona hivi hivi (Fatma Mahamoud)na Sina mda huo (Malkia Leilah Rashid)

Thursday, August 30, 2012

MAPOKEZI YA MBUYU TWITE FUNIKA BOVU

 Akizungumza na waandishi wa habari
 Akiwa na jezi namba 4 iliyokuwa na jina la Rage.
Mashabiki kama kawaida wakimshangilia baada ya kuwasili

MFALME MZEE YUSSUF AKIWA KATIKA DUKA LAKE KARIAKOO

 Big Daddy akionekana kupitia hesabu zake na kuweka mambo sawa ndani ya duka lake.
 Hapa Mfalme akipanga CD za nyimbo mbalimbali zilizotolewa na Jahazi katika duka lake hilo
 Big Daddy, akiweka pozi mbele ya duka lake.
Huyo dada hapo ni mmoja wa wauzaji wa duka hilo, akitabasamu kwa raha zake.

KIONGOZI wa Jahazi na muimbaji mahiri wa kundi hilo, 'Big Daddy' Mzee Yussuf amefungua duka lake pale mjini Kariakoo ambapo anauza vitu mbalimbali zikiwemo CD za bendi hiyo.

Duka hilo, anauza bidhaa mbalimbali ambazo ni pamoja na CD Original za nyimbo za Jahazi, kuna huduma ya DSTV, MP PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY, TTCL, DAWASCO na SASATEL.

Shop hiyo, ambayo ameiboresha vya kutosha ipo njiani kabisa imewekwa mabango mbalimbali yanayoonyesha duka lilipo kama vile MY Entetaiment.

Duka hilo lipo mkono wa kulia kama unatokea mtaa wa Magila karibu na kanisa la KKKT  utakuta mbele kuna hotel ya EMMY utaingia kulia ambapo kama mita 30 utalikuta duka hilo.

Anawakaribisha wateja wote kwenda kupata huduma mbalimbali na mteja hapo ni mfalme anakaribishwa muda wote duka linafunguliwa saa 2.00 asubuhi mpaka jioni. 


'BIG DADDY' AKIWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI

 Hapa ni 'Big Daddy' Mzee Yussuf akiwapa raha mashabiki wake
 Kama kawaida, akiimba kibao cha Mpenzi Chokleti.
 Kanyaga kanyaga komoa komoaaaaa.
 Mfalme akiwa na mcheza kidugu wake Hemedi wakifanya mambo
 Mpaka chini ni kiduku kwenda mbeleeee tu.
 Haya chukue namba yangu. Mzee Yussuf akibadilishana namba na mashabiki wake
Asane tutakupigia mkuu, mashabiki wakimshukuru Mfalme baada ya kuwapa namba yake ya simu.


NA MWANDISHI WETU.

KIONGOZI na muimbaji mashuhuru wa kundi la Jahazi Morden Taarab, Big Daddy Mzee Yussuf, yuko mbioni kutoa albamu yake binafsi hivi karibuni.

Mfalme ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kwa uimbaji na utungaji wa nyimbo za taarabu hapa nchini na nje ya nchi, amesema albamu hiyo itakuwa tishio.

Amesema albamu hiyo kwa sasa iko jikoni na baada ya muda mfupi anatarajia kuipakuwa ambapo amewaomba mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuisubiri albamu hiyo.

Big Daddy, amesema mbali na albamu hiyo binafsi kundi la Jahazi liko katika maandalizi ya mwisho kutoa albamu yake ya 9 ambapo baadhi ya nyimbo zimeshaanza kutungwa.

WAIMBAJI WA JAHAZI WAKIWA KAZINI

 Sauti ya Chiriku, Hadija Yussuf, akitoa burudani.
 Hadija akiwapa raha mashabiki wake.
 'BIG Daddy' Mzee Yussuf, akiwa na dada yake Hadija.
 Nimekuelewa kakaaaaaaaaaaaaaa
 Wanachekaaaaaaaaa, hapo ni Mfalme na Hadija.
 Ni furaha mbele kwa mbeleeeeeeeeeeeeeeeeeee
 Mashabiki wakijimwaya mwaya kwa raha zaoooo.
 Rahaaaaaa, kwa mbeleeeeeee.
 Jamani mumeona kidukuuuuuuuuuu.
 Mfalme akiwajibikaaaaaaaaaa na wacheza kidugu wakeeeeee.
 Haya sasa mambo ya kidugu yakiwa yamenogaaaaaaaaaaaaaa.
Huyuu naye yumooooooooooooooooo

Monday, August 27, 2012

'BIG DADDY' NOMA AJIZOLEA MASHABIKI WA AINA MBALIMBALI

 Biga daddy, Mfalme Mzee Yussuf, akibadilishana namba na mashabiki wake.
 Mashabiki wa Jahazi wakikonga nyoyo zao.
 Zungu uvumilivu ulimshinda na kujichanganya kwenye Jahazi. Hapa akipapasa kinanda.
 Nimekuelewa kaka.
 Amigo akifanya mambo yake.
 Mfalme na Hemed.

Miriamu Amouri akitoa burudani


JAHAZI YAPAGAWISHA MASHABIKI WAKE TRAVETINE USIKU WA LEO

 Malkia Leilah Rashid akitoa Burudani.
 Akijinafasi kwa raha zake.
 Hapa Fatma Alli akifanya majamboziiiii...
 Akikonga nyoyo za mashabiki wake.
 Chezea Fatma weeeee.
 Mtoto Pori ndani ya nyumba.
 Mohamme Alli, akipeana mikono na mashabiki wake.
 Kanyaga kanyaga kanyaga...bong'oa bong'oa.
 Waimbaji wa Jahazi wakiwa stejini.
 Hapa wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali.
 'Big Daddy' akifanya mambo yake.
sauti ya Chiriku Hadija Yussuf akipagawisha mashabiki wake.

NA MWANDISHI WETU.

WAKALI wa mipasho nchini, Jahazi Morden Taarab usiku wa kuamkia leo wamewaacha hoi mashabiki wao baada ya kuwaporomoshea burudani ya jkukata na shoka katika ukumbi wa Travetine Hotel, Magomeni.

Jahazi, wakiongozwa na Mkurugenzi wao, 'Big Daddy' Mzee Yussuf, aliziteka vya kutosha nyoyo za maelfu ya mashabiki waliohudhuria onyesho hilo maalumu.

Onyesho hilo lilikuwa la kwanza baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kufanyika katika ukumbi huo.

Waimbaji wa bendi hiyo, yenye mashabiki wengi kuliko zingine hapa nchini, waliongozwa na Mfalme, Malkia Leilah Rashidi, Hadija Yussuf, Miriamu Amour, Fatma Alli, Abubakari Sudi 'Amigo', Fatma Mahamudu 'Mcharuko'.

Waimbaji wengine waliopamba jukwa katika onyesho hilo, ni Fatma Machupa, Mohammed Alli 'Mtoto Pori', Kidawa, Mwasiti Kitoronto, Mwasiti Mbwana 'MC', Mwanne.

Huku wapapasa kinanda waliongozwa na Chidi Boy, Babu Alli, Tall. Upande wa gita waliongozwa na Director Mudi Maugo, Mussa Bass, Juma Mgunda, Mussa Mussa.