WAKALI wa muziki wa taarab nchini, kundi la Jahazi, linatarajia kuzindua albamu yao ya saba mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza kwa njia ya simu jana Mkurugenzi wa kundi hilo, Mzee Yussuf alisema albamu hiyo inafahamika kwa jina la Mpenzi Chokileti na kwamba itakuwa moto wa kuotea mbali.
Alisema uzinduzi wa albamu hiyo, utaenda sambamba na 'Birthday' ya kundi hilo, itakayofanyika Desemba 24, mwaka huu.
Yussuf alisema kundi hilo limejipanga kikamilifu katika kutoa burudani na amewaomba wapenzi na mashabiki wao kukaa mkao wa kula kwa ajili ya uzinduzi huo.
Baadhi ya albamu zilizowahi kuachiwa na kundi hilo ni pamoja na Wagombanao ndio wapatanao, My Valentain, Daktari wa mapenzi, Two In One, Tupendane na VIP.
Katika hatua nyingine, Yussuf alisema siku ya Idd Mosi kundi hilo linatarajia kuwasha moto maeneo ya Tabata, Dar es Salaam.