Powered By Blogger

Sunday, August 28, 2011

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, inakutana leo mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa iliyotolewa jana mjini Dar es Salaam, na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu, Dar es Salaam, ilisema kikao hicho kitafanyika mchana.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema agenda za mkutano huo ni kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambayo itaenda sambamba na kujadili mapendekezo ya wana CCM wanaoomba kuteuliwa na CCM kugombea jimbo hilo.
Taarifa hiyo ilisema, Pia Kamati Kuu itapokea na kujadili mapendekezo ya wana CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya meya wa manispaa ya Songea kwa tiketi ya CCM.
Ilisema Mukama amesema Kamati Kuu ya CCM, pia itajadili na kuamua kuhusu masuala mengine mbalimbali ya ndani ya Chama hicho.