WAKALI WA MUZIKI WA TAARAB HAPA NCHINI, JAHAZI MORDEN TAARAB 'WANA WA NAKSHI NAKSHI' WAMEANZA MAZOEZI KWA AJILI YA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA ALBAMU YAO YA SABA INAYOTARAJIWA KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI.
MAZOEZI YA KUNDI HILO YAMEANZA JUZI PALE MAGOMENI USALAMA CHINI YA KIONGOZI WA KUNDI HILO MFALME MZEE YUSSUF.
AKIZUNGUMZIA MAZOEZI HAYO MFALME ALISEMA YANAENDA FRESHI NA KWAMBA WAIMBAJI WOTE WANAHUDHURIA KATIKA MAZOEZI HAYO.
ALISEMA MAZOEZIO HAYO PIA NI KWA AJILI YA SHEREHE ZA SIKU KUU YA EID EL-FITR AMBAPO KUNDI HILO LITAFANYA MAONYESHO YAKE SEHEMU MBALIMBALI HAPA JIJINI DAR ES SALAAM.