Powered By Blogger

Wednesday, November 28, 2012

MAZISHI YA SHARO MILIONEA: JIJI LA TANGA LA ZIZIMA

 Mwili wa Marehemu ukishushwa kwenye gari
 Jeneza alilohifadhiwa marehemu Sharo Milionea
Ulinzi ukiimarishwa msibani
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi
 Mama wa Marehemu akilia kwa uchungu
 Mwili ukiwasili makaburini
Mzee Majuto akiwa kwenye majonzi makubwa

VILIO na huzuni vimetikisa katika jiji la Tanga, ambapo msanii na muingizaji wa vichekesho Sharo Milionea alipozikwa jana katika kijiji chao cha Muheza mkoani humo.

Mazishi ya msanii huyo, aliyefariki jana kwa ajili ya gari yalihudhuriwa na maelfu ya wananchi wakiwemo wasanii mbalimbali hapa nchini.

Umati wa wananchi walianza kuhudhuria nyumbani kwao marehemu majira ya asubuhi huku wakiwa na nyuso za manjozi ambapo baadhi yao walishindwa kujizuia na kuangua vilio kwa uchungu.

Msiba wa Sharo Milionea ulishtua wananchi wengi kutokana na nyota ya msanii huyo chipukizi kuanza kungara katika siku za hivi karibuni.

Kiongozi wa Blog hii, Mzee Yussuf na wasanii wengine wa kundi la Jahazi linatoa pole kwa ndugu na jamaa kutokana na msiba huo mzito.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu pahala pema peponi roho ya marehemu. Aminaaa.