Uonane na Fatma Mahamoud Mcharuko
Ufahamiane na mtoto pori Mohamed Ali
Utamuona Big Daddy Mzee Yussuf
Fatma Ali hakosi
Huyu jamaa utamuona pia
Fatma Mahamoud hawezi kuwa nyuma
Hata hawa utawaona ni Muji Maugo na Mussa Mipango
Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf naye atakuepo
Utakutana na Big Daddy na marafiki zake kama hivi
Akiringa na shabiki wake
Hata mtoto wa Mfalme Amigo ataonekana
Director Mudi Maugo na Mwasiti Mbwana wakiongea kama hivi
Asma Machupa utamuona live
Hata Miriamu Amour atakuwa na washikaji zake
Utamuona Asma Machupa na mashabiki wake kama hao
Miriamu Amour utakutana naye
Utamuona Mfalme Mzee Yussuf anavyoimba
Utaonana na mashabiki wastarabu kama hao
Utamkuta Mussa Bezi
Utamuona Malkia Leilah Rashid
Baada ya kupiga kambi katika visiwa vya Zanzibar, wakali wa muziki wa taarab hapa nchini Jahazi usiku huo utakonga nyoyo za mashabiki wao katika ukumbi wa Travetine Hoteli Magomeni mjini Dar es Salaam.
Jahazi itaporomosha burudani katika ukumbi huo kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo chini ya Big Daddy Mzee Yussuf ambapo atazitambulisha nyimbo za albamu yao mpya.
Jahazi itapiga show hiyo ikiwa ni wiki moja sasa baada ya kundi hilo mahiri kukosekana katika ukumbi huo ambapo ilienda katika visiwa vya marashi ya karafu kule Zanzibar kwa ajili ya kufanya maonyesho kadhaa.
Jahazi wameahidi kutoa burudani ya aina yake katika onyesho hili ambapo wamewaomba wapenzi na mashabiki wao kujitokeza kwa wingi usiku wa leo kujionea wenyewe.
Kiongozi wa kundi hilo mahiri hapa nchini Mfalme Mzee Yussuf alisema wamejipanga vya kutosha kwa ajili ya onyesho hilo na amewaahidi wapenzi na mashabiki wao burudani ya aina yake usiku wa leo.