Mkurugenzi Mkuu wa Jahazi 'Big Dady' Mzee Yussuf
Muimbaji mahiri wa Jahazi Fatma Mahamoud 'Mcharuko'
Huyo ndiye Malkia Leilah Rashid kipenzi cha mashabiki wa Jahazi
Hadija Yussuf miongoni mwa waimbaji mahiri wa Jahazi
Mohammed Ali ni muimbaji chipukizi anayetikisa ndani ya Jahazi
Miriamu Amour muimbaji mwenye mahiba maridhawa
Asma Machupa kinda wa Jahazai Morden anayepagawisha mashabiki
Fatma Ali ni muimbaji mahiri wa kutegemewa
Aboubakary Sudi 'Amigo' kichwa kimoja mashabiki elfu moja
Mwasiti Kitoronto ni muimbaji makini na anayejiamini muda wote
Babu Ali mpiga kinanda mashuhuri wa Jahazi Morden
Huyo ni Mussa Mipango hakika ni mpiga gita la solo mashuhuri hapa nchini
Mgeni Saidi mpapasa kinanda anayejiamini
Dk. Mudi Mauji directior wa Jahazi anayetesa kwa kuchana nyuzi
Mauji tena
Ni mpiga solo mpya wa Jahazi
Waimbaji mahiri wa bendi ya Jahazi
Hao ndio wakali wa gita la solo ndani ya Jahazi
Huyo ni Mzee Yussuf akiwa na Hamis Boha (kushoto) ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa Jahazi
DIrector Maugo akimpa maelekezo Mwasiti MC
Mshika fedha wa bendi Seif Mwagwaru akicheza na Amigo
Hao ni miongoni mwa mashabiki wa Jahazi
Miongoni mwa mashabiki wa bendi
Huyo ni Fatma Ali akiimba
Hapa ni Hadija Yussuf na Muhamed Maugo
Malkia Leila Rashid akiiwapa raha mashabiki
Miriamu Amour na mashabiki wake
Mfalme Mzee Yussuf akiwamba mbele ya umati wa mashabiki wake
Seif akimtunza Mussa Mipango
Hiyo ni sehemu ya mashabiki wa Jahazi Morden Taarab
Shabiki akicheza na Mussa Bezi kwa raha zake kabisa
Huyo ni mnenguaji wa kundi la Khanga moja anaitwa Zawiya akiwa katika show ya Jahazi
Mfalme na mashabiki wake
Hadija Yussuf akitoa burudani
Fatma Mcharuko akiimba
Mohamed Ali akinogesha
Wacheza viduku kama kawaida
Mcharuko akishiriki kucheza kiduku
Chid boy akipapasa kinanda
HISTORIA FUPI YA BENDI
Jahazi Morden Taarab 'Wana wa nakshinakshi' ni bendi ya muziki wa taarab yenye mashabiki wen gi wengi zaidi kuliko bendi nyingine zozote hapa nchini.
Bendi hii ndio walioanzisha kupiga muziki wa kisasa 'modern' na kufuatiwa na bendi nyingine ambazo hadi sasa zinasuasua.
Jahazi ni bendi in ayomilikiwa na Mzee Yussuf 'Mfalme' ambaye aliianzisha baada ya kutesa kwenye makundi ya Zanzibar Stars na East Afrika Melody kipindi hicho.
Bendi hii ilizinduliwa katika ukumbi wa Travetine Magomeni, Dar es Salaam ambapo hadi sasa ndio ukumbi wake wa nyumbani na maskani ya bendi hii yapo Magomeni pia.
Kundi hili lilizinduliwa mwaka 2006 na hadi sasa limezindua albamu kali nane (8) ambazo zinaendelea kutamba hadi sasa.
Jahazi imekuwa kifanya maosheso yake nchi mzima bila ya kujali umbali wa nchi yetu pia hufanya maonyesho kwenye nchi mbalimbali duniani.
Kundi hili limesheheni wasanii mahiri wengi wakiwemo Hadija Yussuf, Leila Rashid, Fatma Mcharuko, Miriamu Amour, Amigo, Mohamed Ali, Mwasiti Mbwana, Mwasiti MC, Fatma Ali, Asma Machupa, Kidawa, Fatma Kasimu,.
Wapigaji yumo Babu Ali, Chidi boy, Musaa Bezi, Musa Mipango, Mudi Maugo, Tall, na wengine wengi.
Jahazi ndio bendi pekee inayomiliki timu ya mpira wa miguu inayoitwa Jahazi FC chini ya Hamis Boa ambaye anaiongoza kwa sasa.
Bendii hii usiku huu itafanya onyesho lake katika ukumbi wa nyumbani wa Travetine Hotel uliopo Magomeni Dar es Salaam.