Powered By Blogger

Tuesday, November 27, 2012

SHAROMILIONEA AMEFARIKI DUNIA.

 Sharo
 Sharomilionea enzi za uhai wake
Mzee Majuto na Sharomilionea enzi za uhai wake

PIGO

TATHINIA ya filamu nchini imepata pigo baada ya msaani nguli Sharobilionea kufariki dunia  jana katika ajali ya gari.

Sharo ambaye amejipatia umaarufu siku za karibuni alifariki baada ya gari lake kupinduka wakati akielekea Tanga eneo la Segera.

Blog hii tutatoa pole kwa ndugu na jamaa na marafiki na mungu aiweke roho ya marehemu pahala pema peponi amina.  

Habari ambazo zimetufikia hivi punde zinapasha kwamba muigizaji na mwanamuziki, Hussein Ramadhan Mkieti almaarufu kama Sharo Milionea,amefariki dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea mida ya saa mbili usiku katika eneo la Maguzoni Songa katikati ya Segera na  Muheza mkoani Tanga.
Habari za ajali hii na tukio hili la kusikitisha zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Masawe. Kwa mujibu wa Kamanda huyo, gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BBR alilokuwa akiendesha marehemu kutokea Dar-es-salaaam kwenda Muheza lilipofika katika eneo hilo liliacha barabara na kupinduka na hivyo kusababisha mauti yake.Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali Teule ya Muheza.
BC inaungana na wapenzi wote wa sanaa nchini Tanzania kutoa pole za dhati kwa ndugu,jamaa na marafiki wa Sharo Milionea.Pumzika kwa Amani.

Read more: BREAKING NEWS: SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA! - BongoCelebrity