Powered By Blogger

Thursday, January 31, 2013

Usajili wa Drogba wapingwa na klabu yake

Didier Drogba

Klabu ya Shanghai Shenhua imesema kuwa Didier Drogba angali mchezaji wake na kuwa uhamisho wake hadi klabu ya Galatasaray inakiuka masharti ya mkataba wake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea, amesaini mkataba wa miezi kumi na minane na klabu ya Galatasaray inayoshiriki katika ligi kuu ya Uturuki.

''Tumeshangazwa sana na tangazo hilo'' Klabu hiyo ambayo ilimsaini Drogba kwa mkataba wa miaka miwili na nusu mwezi Julai mwaka uliopita, imesema.

''Drogba angali mchezi wa klabu ya Shanghai Shenhua kwa kuwa mkataba kati yao bado haujakamilika.

Klabu ya Galatasaray siku ya Jumanne ilitangaza kuwa Drogba atajiunga na klabu hiyo baada ya kukamilika na mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Afrika Kusini.

Lakini Shenhua imepinga uhamisha huo na kussema kuwa liko tayari kuwasilisha malalamishi yake ya shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.

Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.

Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa na kampuni ya uhusiano bora inayomuakilisha mchezaji huyo Sports PR Company na kuchapishwa kwa mtandano wa kijamii wa Twitter, Drogba alisema anajiandaa kurejea tena katika michuano ya kuwania kombe la klabu binga barani ulaya kwa mara nyingine.

Galatasaray imefuzu kwa raundi ya muondoana ya kuwania kombe hilo na imepangiwa kucheza na FC Schalke 04 kutoka uUjerumani.

''Hii ni fursa nzuri ya kuichezea timu kubwa na ni nafasi ambayo siwezi kupuuza'' Alisema Drogba.