KIONGOZI wa Kundi la Jahazi, Mzee Yussuf ameondoka nchini leo kuelea Ulaya kwa ajili ya kufanya maonyesho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, kiongozi huyo, aliyejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi baada ya kuwa mtu wa kwanza kuibadilisha sanaa ya taarab kwa kupiga taarab ya kisasa yaani 'Morden' atafanya maonyesho ya siku mbili tatu na kurejea nyumbani.
Jahazi hizi sasa inajiandaa na uzinduzi wa albamu yao mpya inayofahamika kwa jina la 'Mpenzi Chokileti' ambayo itazinduliwa Desemba 24, mwaka huu, na itakwenda sambamba na 'birthday' ya kundi hilo.
Kwa mujibu wa Mfalme albamu hiyo inatakuwa na nyimbo sita na tayari zimeshaanza kupigwa kwenye baadhi ya kumbi za burudani.
Mzee Yussuf aliongeza kuwa kundi lake hivi sasa liko katika hali mzuri na limesheheni wasanii kibao na kwamba wako katika hatua za mwisho kupata msaanii mpya ambaye hakutaka kumtaja kwa sasa.
Jahazi hivi sasa inatamba na albamu ya wagombanao ndio wapatanao.