BREKING NEWZZZ. ZAIDI ya
watu 500 wanasadikiwa kufariki
dunia baada ya meli waliokuwa
wakisafiria kutoka Unguja
kwenda Pemba kuzama katika
bahari ya Nungwi.
Meli hiyo ilikuwa imechukua abiria
zaidi ya 610 pamoja na mizigo
ilizama usiku wa kuamkia leo saa
8.30 baada ya kutokea hitilafu.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizopatikana kutoka Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk. Alli
Mohammed Sheni yupo eneo la
tukio kuangalia jinsi uokoaji
unavyoendelea.
Taarifa pia, zilisema juhudi za
kuokoa waliozama katika meli
hiyo zinaendelea ambapo
wanaokolewa wanapelekwa
katika viwanja vya Maisara kwa
ajili ya kutambuliwa na ndugu
zao.
Tutaendelea kuwaletea taarifa
hapo baadae.