Powered By Blogger

Sunday, February 19, 2012

MFALME MZEE YUSSUF KUWASHA MOTO DAR LIVE MBAGALA

Marchi mbili mwaka huu, wapenzi wa muziki wa taarab nchini wanaisubiria kwa hamu hususan wale wanaoingia katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala.

Siku hiyo wapapasa vinanda maarufu akiwemo Mfalme Mzee Yussuf (Jahazi), Ally Jay (5stars) na Thabit Abdul (Mashauzi Classic) watakapochuana katika mpambano wa kupapasa vinanda.

Mpapano huo umepangwa kufanyika katika ukumbi huo na kila mtu hivi sasa anazungumzia mpambano huo.