Mfalme Mzee Yussuf akipapasa.
Maelfu ya mashabiki wa muziki wa taarab hususan wale wa Jahazi wanamsubiri kwa hamu muimbaji na mkurugenzi wa kundi hilo, Mzee Yussuf aliyeko katika Jiji la Washington Dc-Marekani kikazi. Kiongozi huyo yuko nje ya nchi kwa majuma kadha sasa na anatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa.Ujio wa nguli huyo wa taarab unasubiriwa kwa hamu na wapenzi na mashabiki wake ambao wamepanga kumpokea kwa shangwe, nderemo na vifijo katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasili nchi kiongozi huyo amepangiwa kufanyiwa sherehe ya aina yake iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa travetine hoteli Magomeni.