Powered By Blogger

Tuesday, February 21, 2012

MTOTO PORI AKIJANAFASI KWA RAHA ZAKE

Muimbaji chipukizi wa kundi la Jahazi, Mohammed Ally 'Mtoto Pori' akiweka pozi wakati wa onyesho la kundi hilo.

MWASITI KITORONTO AKITOA BURUDANI

Muimbaji nguli wa kundi la Jahazi Mwasiti Kitoronto akionyesha uwezo wake mbele ya mashabiki wa kundi hilo.

KIDUKU MBELE KWA MBELE

Wacheza kiduku wakitoa burudani katika show hiyo

MCHARUKO AKIKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE

Fatma Mahamuod 'Mcharuko' akijinafasi na mashabiki wake hawapo pichani

NATURE KUPAMBA ONYESHO LA JAHAZI MTONI GRILL.

Juma Kasimu Nature 'Kibla'

Monday, February 20, 2012

TUPO KAZINI

Mashoti hawa wakipitia magazeti baada ya kufika ofisini.

Sunday, February 19, 2012

Mfalme Mzee Yussuf akipapasa.

Maelfu ya mashabiki wa muziki wa taarab hususan wale wa Jahazi wanamsubiri kwa hamu muimbaji na mkurugenzi wa kundi hilo, Mzee Yussuf aliyeko katika Jiji la Washington Dc-Marekani kikazi. Kiongozi huyo yuko nje ya nchi kwa majuma kadha sasa na anatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa.Ujio wa nguli huyo wa taarab unasubiriwa kwa hamu na wapenzi na mashabiki wake ambao wamepanga kumpokea kwa shangwe, nderemo na vifijo katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasili nchi kiongozi huyo amepangiwa kufanyiwa sherehe ya aina yake iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa travetine hoteli Magomeni.

JAHAZI KUJIVINJARI TRAVE USIKU WA LEO

Wakali wa muziki wa taarab, Jahazi watajivinjari na mashabiki wao leo katika ukumbi wa travetine hoteli Magomeni, Dar es Salaam, onyesho hilo limepangwa kuanza saa tatu usiku na kundi hilo litapiga vibao vyao vyote vikali kikiwemo cha 'Mpenzi Chokleti'.

DAR MORDEN TAARAB KUPAKUA ALBAMU TATU KWA MPIGO

Kundi la taarab la Dar Morden Taarab 'Watoto wa Kandoro, wajukuu wa Makamba' wanatarajia kupakua albamu tatu kwa mpigo. Albamu hizo wanatarajia kuzipakua Ijuma ya Marchi 2 mwaka huu, katika ukumbi wa Travetine Hoteli, Magomeni Dar es Salaam.

KKatika uzinduzi huo uliopangwa kuanza saa tatu usiku, utasindikizwa na kundi la Baikoko kutoka Tanga na Kanga Moja la DSM.

MFALME MZEE YUSSUF KUWASHA MOTO DAR LIVE MBAGALA

Marchi mbili mwaka huu, wapenzi wa muziki wa taarab nchini wanaisubiria kwa hamu hususan wale wanaoingia katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala.

Siku hiyo wapapasa vinanda maarufu akiwemo Mfalme Mzee Yussuf (Jahazi), Ally Jay (5stars) na Thabit Abdul (Mashauzi Classic) watakapochuana katika mpambano wa kupapasa vinanda.

Mpapano huo umepangwa kufanyika katika ukumbi huo na kila mtu hivi sasa anazungumzia mpambano huo.

SIMBA, KIYOVU NGUVU SAWA

Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic.

Saturday, February 18, 2012

HAPITI MTU HAPA.

Beki wa Yanga Athuman Iddi Chuji, akimzuia mshambuliaji wa Zamalek.

YANGA, ZAMALEK NGUVU SAWA

Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiza akiomba dua baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Zamalek, timu hizo zilitoka uwanjani kwa kufungana bao moja kwa moja.mchezo ulipigwa uwanja wa Taifa.

Friday, February 17, 2012

YANGA KUIVAA ZAMALEKI KESHO

Kikosi cha Yanga kesho kitashuka dimbani kuvaana na
timu ya Zamaleki kuwania kufuzu klabu bingwa Afrika.

Yanga itashuka uwanjani ikiwa na matumaini makubwa ya ushindi kutokana na kufanya maandalizi ya kutosha.

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Wednesday, February 15, 2012

FATMA MCHARUKO: JAHAZI IMENIPA UMAARUFU MKUBWA KIMUZIKI

FATMA MCHARUKO AKIWA NA WASANII WENZAKE WA JAHAZI

NGULI WA MUZIKI WA TAARAB, FATMA MAHAMUOD 'MCHARUKO' AMESEMA WIMBO WA MTANIONA HIVI HIVI UMEMPATIA UMAARUFU MKUBWA KATIKA MEDANI YA MUZIKI HAPA NCHINI.

MCHARUKO NASEMA KIBAO HICHO KIMEMFANYA KUFAHAMIKA SEHEMU NYINGI NA KUJIONGEZEA UMAARUFU KUPITIA KAZI HIYO.

MUIMBAJI HUYO ANAYESHIKA MAIKI KATIKA BENDI YA JAHAZI CHINI YA MFALME MZEE YUSSUF ANASEMA ANAMSHUKURU KIONGOZI HUYO WA JAHAZI KWA KUMFANYA AFIKE HAPO ALIPO.

AKIZUNGUMZIA KUNDI HILO ANASEMA BADO ANAIMANI KUWA NDIO KUNDI PEKEE LENYE KUTOA BURUDANI YA MUZIKI WA TAARAB HAPA NCHINI NA KUWAKONGA MASHABI WENGI.

MCHARUKO ALIYEWAHI KUTAMBA NA WIMBO WA MFAMAJI HIVI SASA AMEPANGA MIKAKATI MINGI IKIWA NI PAMOJA NA KUJITUMA KWA BIDII ILI AWEZE KUPATA MAFANIKIO MENGI ZAIDI.

IMEANDALIWA NA MOHAMMED ISSA.

KIONGOZI WA JAHAZI MZEE YUSSUF (KATIKATI) AKIWA NA WENYEJI WAKE MAREKANI

ICON WA MUZIKI WA TAARAB MZEE YUSSUF AKILAKIWA NA WENYEJI WAKE MARA BAADA YA KUWASILI JIJINI WASHINGTON DC MAREKANI, HUYO HUKO KWA AJILI YA KUFANYA MAONYESHO KADHAA NA ANATARAJIWA KUWASILI MUDA WOWOTE KUTOKA SASA.

MZEE YUSSUF, ALLY JAY NA THABITI ABDULL NANI MKALI WA KUPIGA KINANDA?




JUU NI MFALME MZEE YUSSUF NA CHINI NI ALLY JAY.WANATARAJIA KUPANDA JUKWAA MOJA MARCH 2 MWAKA HUU,KUMTAFUTA MKALI WA KUPAPASA KINANDA TANZANIA?

MTU MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI


WATAALAMU WA MAKUMBUSHO WAKIMPIMA UREFU MTU ANAYEDHANIWA KUWA MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI. MTU HUYO ANAISHI INDIA NA ANAUREFU WA SENTI MITA 20



RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATA AKIWA NA WANACHIPOLOPOLO

RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATA AKIKABIDHIWA KOMBE LA AFRIKA IKULU NCHINI HUMO, BAADA YA WANACHIPOPOLO KUNYAKUA UBINGWA WA AFRIKA HIVI KARIBUNI.

KAMATI YA CHEYO YAIBANA SERIKALI

MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE, HESABU ZA SERIKALI, JOHN CHEYO.

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC), IMEIBANA SERIKALI NA KUITAKA KUWEKA WAZI MATUMIZI YA FEDHA ZINAZOCHANGWA KWA AJILI YA WAHANGA WA MAAFA HAPA NCHINI.

WAJUMBE WA PAC WALISEMA HAYO JANA WALIPOKUTANA NA WATENDAJI KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWENYE OFISI NDOGO ZA BUNGE DAR ES SALAAM.



YANGA USO KWA USO NA ZAMALEKI


KIKOSI CHA TIMU YA YANGA
MABINGWA WA TANZANIA BARA YANGA INATARAJIA KUVAANA NA MIAMBA YA ZAMALEKI KATIKA MCHEZO KLABU BINGWA AFRIKA ULIOPANGWA KUFANYIKA 18.2.2012 NA KUPIGWA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.

MFAMLE MZEE YUSSUF KUPOKEWA KWA SHANGWE