Powered By Blogger

Monday, May 28, 2012

KUNDI la muziki wa mwambao la Jahazi limeahidi kuendelea kutoa burudani yenye kiwango cha hali ya juu na imewashukuru wapenzi na mashabiki wake kwa kuliunga mkono kundfi hilo mahiri la taarab hapa nchini.

Ahadi hiyo imetolewa na mkurugenzi wa kundi hilo Mfalme Mzee Yussuf alipokuwa akizungumza na mwandishi wa blog hii jijini Dar es Salaam.

Mfalme alisema kundi hilo ambalo hivi sasa limejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kupiga burudani ya aina yake inayowasisimua wapenzi na mashabiki wao.

Alisema Jahazi itaendelea kuwapa raha wapenzi na mashabiki wao na kundi hilo litaendelea kuwapa raha kwa kuimba na kutunga nyimbo zinazoenda na wakati.