Powered By Blogger

Sunday, March 24, 2013

Jahazi kutibwirika trave usiku huu

Kiongozi wa Jahazi Mfalme Mzee Yussuf

Kundi la Jahazi usiku huu litaachia burudani ya kukata na shoka katika ukumbi wake wa nyumbani uliopo travetine hotel, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Wakiongozwa na Mfalme Mzee Yussuf, waimbaji wa Jahazi watapanda jukwaani kwa moyo wa furaha na shauku kubwa kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wao

Thursday, January 31, 2013

WENGER SINA MPANGO WA KUMSAJILI BECKHAM

David Beckham

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, amepuuzilia mbali madai kuwa anapanga kumasajili aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham, baada ya kumruhusu mchezaji huyo kufanya mazoezi na klabu yake.

Beckham, 37, hana klabu tangu alipokihama klabu ya Los Angeles Galaxy mwisho wa msimu uliopita.

Wenger alisema, mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alimpigia simu kuuliza ikiwa anaweza kufanya mazoezi na Arsenal.

Beckham hajacheza mechi yoyote tangu mwezi Decemba wakati alipoisaidia klabu yake ya LA Galaxy kuhidhafi kombe la MLS kwa mwaka wa pili mfululizo, kufuatia ushindi wao wa magoli matatu kwa moja dhidi ya Houstan Dynamo.

Mchezaji huyo alikuwa amehusishwa na vilabu ya Paris Saint Germain na Monaco, lakini baada ya mechi hiyo alisema kuwa hana uhakika ni klabu ipi ataichezea.
Bechkam aliicheza timu ya taifa ya Uingereza mechi mia moja na kumi na tano na mwara ya mwisho ni mechi kati ya Uingereza na Belarus Oktoba mwaka wa 2009.

Usajili wa Drogba wapingwa na klabu yake

Didier Drogba

Klabu ya Shanghai Shenhua imesema kuwa Didier Drogba angali mchezaji wake na kuwa uhamisho wake hadi klabu ya Galatasaray inakiuka masharti ya mkataba wake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea, amesaini mkataba wa miezi kumi na minane na klabu ya Galatasaray inayoshiriki katika ligi kuu ya Uturuki.

''Tumeshangazwa sana na tangazo hilo'' Klabu hiyo ambayo ilimsaini Drogba kwa mkataba wa miaka miwili na nusu mwezi Julai mwaka uliopita, imesema.

''Drogba angali mchezi wa klabu ya Shanghai Shenhua kwa kuwa mkataba kati yao bado haujakamilika.

Klabu ya Galatasaray siku ya Jumanne ilitangaza kuwa Drogba atajiunga na klabu hiyo baada ya kukamilika na mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Afrika Kusini.

Lakini Shenhua imepinga uhamisha huo na kussema kuwa liko tayari kuwasilisha malalamishi yake ya shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.

Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.

Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa na kampuni ya uhusiano bora inayomuakilisha mchezaji huyo Sports PR Company na kuchapishwa kwa mtandano wa kijamii wa Twitter, Drogba alisema anajiandaa kurejea tena katika michuano ya kuwania kombe la klabu binga barani ulaya kwa mara nyingine.

Galatasaray imefuzu kwa raundi ya muondoana ya kuwania kombe hilo na imepangiwa kucheza na FC Schalke 04 kutoka uUjerumani.

''Hii ni fursa nzuri ya kuichezea timu kubwa na ni nafasi ambayo siwezi kupuuza'' Alisema Drogba.

Sunday, January 20, 2013

Chelsea yairarua Arsenal, mechi bado inaendelea

Frank Lampard

Chelsea imeimarisha nafasi yake ya kusonga mbele kwenye msururu wa ligi kuu ya premier kwa kuilaza Arsenal magoli mawili katika muda 20 ya kipindi cha kwanza ya mechi yao inayoendelea katika uwanja wa Stampford Bridge.

Juan Mata alipachika bao la kwanza la Chelsea kabla ya Frank Lampard kufunga bao la pili kupitia kwaju wa penalti.

Kipa wa Arsenal alimuangusha Ramires ndani ya kijisanduki na kumlazimisha refa wa mechi hiyo kutoa adhabu ya penalti na pia kuumpa kipa huyo kadi ya njano.

Mechi hiyo inaendelea sasa.

Mzee Yussuf kuunguruma Travetine usiku huu

'Big Daddy' Mzee Yussuf

Kiongozi wa Jahazi Mfalme Mzee Yussuf usiku huu atakonga nyoyo za mashabiki wake katika ukumbi wa Travetine Hoteli Magomeni.

Mzee Yussuf akiwa na waimbaji wake wote mahiri watapanda jukwaani katika onyesho lao kabambe litakaloanza saa tatu usiku mpaka majogoo.

Onyesho hilo, Jahazi litapiga nyimbo zake zote zinazotamba na zile zilizotamba ambazo bado zinawika kwenye viunga mbalimbali vya burudani ndani na nje ya nchi.


Ratiba ya Michuano ya Kombe la Afrika inayoendelea Afrika Kusini
Soma chini ujue ratiba ya michuano hiyo.

Ratiba ya mashindano ya kandanda ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini. Tarehe 19 Januari hadi 10 Februar.

Taarifa zinazohusianaMichezoNyakati zote ni Afrika Mashariki


Group A:1.Angola | P: 1 | Pointi: 12. Cape Verde | P: 1 | Pointi:13. Morocco | P: 1 | Pointi: 14. South Africa| P: 1 | Pointi: 1Matokeo ya mechi za kundi A19/01/2013 Afrika Kusini 0 Cape Verde 0
19/01/2013 Angola 0 Morocco 0
________________________________________
23/01/13:
Afrika Kusini dhidi ya Angola (Saa Kumi na mbili Jioni)
Morocco dhidi ya Cape Verde (Saa Tatu za Usiku)
27/01/13:
Afrika Kusini dhidi ya Morocco (Saa Mbili za Usiku)
Cape Verde dhidi ya Angola (Saa Mbili za Usiku)
Group B1. Ghana | P: 0 | Pointi: 0
2. Mali | P: 0 | Pointi: 0
3. Niger | P: 0 | Pointi: 0
4. DR Congo | P: 0 | Ponti: 0
_________________________________________________________
20/01/13:
Ghana dhidi ya DR Congo (Saa Kumi na Mbili za Jioni)
Mali dhidi ya Niger (Saa Tatu za Usiku)
24/01/13:
Ghana dhidi ya Mali (Saa Kumi na Mbili za Jioni)
Niger dhidi ya DR Congo (Saa Tatu za Usiku)
28/01/13:
Ghana dhidi ya Niger (Saa Mbili za Usiku)
DR Congo dhidi ya Mali (Saa Mbili za Usiku)
Group C1. Zambia | P: 0 | Pointi: 0
2. Nigeria | P: 0 | Pointi: 0
3. Ethiopia | P: 0 | Pointi: 0
4. Burkina Faso | P: 0 | Pointi: 0
_________________________________________________________
21/01/13:
Zambia v Ethiopia (Saa Kumi na Mbili Jioni)
Nigeria v Burkina Faso (1 (Saa Tatu za Usiku)
25/01/13:
Zambia dhidi ya Nigeria (Saa Kumi na Mbili za Usiku)
Burkina Faso dhidi ya Ethiopia (Saa tatu za Usiku)
29/01/13:
Zambia dhidi ya Burkina Faso (Saa Mbili za Usiku)
Ethiopia dhidi ya Nigeria (Saa Mbili za Usiku)
Group D1. Ivory Coast | P: 0 | Pointi: 0
2. Algeria | P: 0 | Pointi: 0
3. Tunisia | P: 0 | Pointi: 0
4. Togo | P: 0 | Pointi: 0
_________________________________________________________
22/01/13:
Ivory Coast dhidi ya Togo (1500) ()
Tunisia dhidi ya Algeria (1800) ()
26/01/13:
Ivory Coast dhidi ya Tunisia (1500) ()
Algeria dhidi ya Togo (1800) ()
30/01/13:
Ivory Coast dhidi ya Algeria (Saa Mbili za Usiku)
Togo dhidi ya Tunisia (Saa Mbili za Usiku)
Quarter-finals02/02/13:

Mshindi wa kundi B kupambana na timu ya pili kundi A (Saa Kumi na Mbili za Usiku)
Mshindi wa kundi A kumbana na timu ya pili kundi B (Saa tatu na nusu za Usiku)
03/02/13:
Mshindi wa kundi D dhidi ya timu ya pili kundi C (Saa Kumi na mbili jioni)
Mshindi wa kundi C dhidi ya timu ya pili kundi D ( (Saa tatu na nusu za Usiku)
Semi-finals06/02/13:
Mshindi wa robo fainali ya pili dhidi ya mshindi wa robo fainali ya tatu saa (Saa Mbili za Usiku)
Mshindi wa robo fainali ya nne dhidi ya mshindi wa robo fainali ya kwanza (Saa tatu na nusu za Usiku)

Timu itakayoshindwa katika mechi ya nusu fainali (Saa tatu Usiku)
Final 10/02/13:

Washindi wa mechi ya nusu fainali (Saa Tatu za Usiku

Michuano ya Afrika: Angola, Morocco ngoma inogile


Kikosi cha Angola

Kikosi cha AngolaAngola imetoka sare ya kutofungana bao lolote na Morocco katika mechi ya pili ya michuano ya fainali ya kombe la mataifa ya Afrika, iliyoanza nchini Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya pili ya kundi A ilichezwa katika uwanja wa Soccer City,mjini Durban na Angola walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Juhudi za mshambulizi matata wa Angola wa timu ya Real Valladolid, Manucho za kupachika magoli, hazikuzaa matunda, licha ya vijana hao wa Angolaa kuthibiti mpira wa asilimia kubwa.
Kocha wa Angola, Gustavo Ferrin amesema timu hiyo ipo katika mashindano hayo kwa malengo na amesema kuwa amefurahia matokeo ya mechi hiyo.

Naye kocha wa Morocco, Rachid Taoussi, kwa upande wake amesema hamasa ya timu yake ni kufika hatua ya mbele zaidi ya mashindano hayo.

Kufuatia matokeo hayo timu zote katika kundi A zina alama moja kila mmoja baada ya mechi ya ufunguzi katika ya wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde kumalizika kwa timu hizo pia kutoka sare ya tasa.

Manchester City yailaza Fulham mbili


Luis Suarez

David Silva alifunga magoli mawili na kuisadia Manchester City, kuilaza Fulham katika uwanja wao wa Etihad na kupunguza idadi ya alama kati yao na vinara wa sasa Manchester United.
Kufuatia ushindi huo, wa magoli mawili kwa bila mabingwa hao watetezi wako alama nne nyuma Manchester United.
United hata hivvyo inaweza kurejesha uongozi wao wa alama saba hapo kesho ikiwa watashinda mechi yao dhidi ya Tottenham.
Katika mechi nyingine, kwa mara ya kwanza washambulizi wa Liverpool Luis Suarez na Daniel Sturridge walicheza pamoja katika mechi moja na kila mmoja wao kufunga bao wakati wa mechi yao dhidi ya Norwich.
Liverpool ilishinda mechi hiyo kwa kuinyuka Norwich magoli matano kwa yai.

Luis Suarez
Newcastle nayo ilipoteza alama tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumabani pale ilipolimwa magoli mawili kwa moja na Reading.
Adam Le Fondre ambaye aliingia kama mchezaji wa ziada alifunga magoli mawili katika muda wa dakika sita.
Kufuaia kipigo hicho, Newcastle sasa imeshuka hadi nafasi ya 17 na alama 21.
Newcastle hata hivy7o ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa mshambulizi wake Yohan Cabaye.
Jonathan de Guzman alifunga magoli mawili naye Ben Davies akafunga bao moja na kuhakikishia Swansea, alama tatu muhimu za ligi kuu ya premier.
Swansea iliinyeshea Stoke City magoli matatu kwa moja.
Katika matokea mengine West Ham ilitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na QPR nayo Wigan ikafunga magoli 2 - 3 na Sunderland.


Mfahamu Sitti bint Saad mwanamke wa kwanza kuimba taarab hapa nchini

Sitti bin Saad

SITI Bint Saad ni mwimbaji mkongwe nchi aliyetokea kwenye familia dunia ambaye alibarikiwa kipaji cha pekee cha uimbaji.

Kipaji cha muimbaji huyo kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza.

Siti alijaliwa kuwa na sauti iliyoweza kupaa na kusafiri kwa umbali wa maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vyao vinapita.

Nguli huyo alifananishwa kuwa na mapafu yenye nguvu kama simba kutokana na alivyoweza kupaza sauti yake mbali bila kuachia pumzi.

Historia inaonyesha kwamba Siti alizaliwa katika kijiji cha Fumba, Zanzibari mwaka 1880 na baada ya kuzaliwa alipewa jina la 'Mtumwa' kwasababu alizaliwa katika kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na mkabaila mmoja wa kiarabu.

Baba yake Mzee Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa ni Mzigua toka Tanga, lakini wote wawili walizaliwa Zanzibari.

Hali ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha zaidi katika shughuli za kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri.

Kama waswahili wasemavyo 'kuzaliwa masikini si kufa masikini' Siti kipaji cha uimbaji alichobarikiwa muimbaji huyo kilimsaidia siku za awali za maisha yake na alitumia kipaji hicho kuuza vyungu vya mama yake.

Kutokana na wakati huo elimu kwa watoto wa kike kutotiliwa mkazo, Siti hakuwahi kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya kusoma Kurani.

Mnamo mwaka 1911 alihamia mjini ili kubooresha maisha yake.Ujio wake wa kuishi mjini ulikuwa wa neema kwani ulimkutanisha na muimbaji wa kundi la muziki wa taarabu la "Nadi Ikhwani Safaa" Muhsin Ali.

Katika kipindi hicho, kundi la Nadi Ikhwani Safaa lilikuwa kundi pekee la muziki wa taarabu lililoanzishwa na Sultani mpenda starehe na anasa Seyyid Barghash Said.
Kundi hilo lilikuwa la wanaume peke yake , wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na vikundi vya muziki kwani ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni.

Hata hivyo Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Siti na hivyo akajitolea kumfundisha kuimba kwa kufuata vyombo vya muziki na lugha ya kiarabu.

Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenziwe wa Nadi Ikhwani Safaa ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonyesho mbalimbali katika jamii.

Walipata mialiko mingi iliyokuwa ikitoka kwa Sultani na matajiri wengine wa kiarabu na walimtumia kwenye maonyesho mengine yakiwemo ya harusi.

Inasemekana ulifika wakati ambapo sherehe zilishindwa kufana kama Siti hakuwepo kutumbuiza kwani alikuwa moto wa kuotea mbali na jina lake lilivuma kwa haraka hadi nje ya mipaka ya nchi na bara la Afrika.

Hali hiyo ilisababisha Siti afananishwe na muimbaji wa kike aliyetamba wakati huo kutoka Misri Umm Kulthum.

Mwaka 1928 kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's voice yenye makazi yake Mumbai India ilisikia umaarufu wa muimbaji huyo na ikamwalika pamoja na kundi lake kwenda kurekodi kwa lugha ya Kiswahili ili kujaribu kama muziki wake utauzika.

Kampuni hiyo haikuweza kuamini jinsi muziki ule ulivyouzika kwa kasi kubwa kwani wastani wa santuri 900 ziliweza kuuzwa katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo na hadi kufikia 1931 santuri 72,000 zilikuwa zimeuzwa.

Kutokana na kusambaa kwa santuri hizo umaarufu wa Siti ulizidi mara dufu watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walifika Zanzibari kuja kumwona muimbaji huyo.

Mambo yalizidi kuwa mazuri kwa Siti hadi ikafikia hatua kampuni ya kurekodi ya Columbia kuamua kujenga studio ya kurekodi muziki Zanzibar mahususi kwa muimbaji huyo.

Hatua ya kujengewa studio hiyo iliwaumiza wengi wenye wivu na wakaanza kumtungia nyimbo za kumkejeli ili kumshusha na hasa walitumia kigezo kwamba hana uzuri wa sura, nyimbo nyingi ziliimbwa lakini huo ndio uliovuma sana.



BI KIDUDE NGULI WA TAARAB MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akimvisha tuzo Fatma bint Baraka 'Bikidude'.

FATMA binti Baraka 'Bikidude' ni miongoni mwa wasanii wakongwe hapa nchini wenye historia ya kipekee. Licha ya kuwa na historia ya kipekee, msanii huyo mkongwe amejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kupitia kazi yake ya sanaa.

Bikidude anaminika kwamba ndie msanii mkongwe kuliko msanii mwingine yoyote wa kike hapa nchini.

Msanii huyo ni muimbaji mwenye historia ya kipekee hapa nchini na kutokana na umahiri wake wa uimbaji na amefanikiwa kutembea nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Asia kwa ajili ya kufanya kazi zake za muziki na kuitangaza taifa kwenye jumuia za kimataifa.

Katika siku za hivi karibuni, mkongwe huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi lakini kwa sasa hali yake inaendelea vizuri ingawa hajaanza kufanya shughuli zake za muziki.

Katika makala haya nitazungumzia historia fupi ya msanii huyo ambaye mwishoni mwa mwaka jana, serikali ilimtunukia nishani ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa kwa taifa. Nishani hiyo alitunukiwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu mjini Dar es Salaam.

Rais Kikwete alimtunuku Bikidude na wasanii wengine nishani ya sanaa na michezo ambayo hutolewa kwa wasanii na wanamichezo mashuhuri, ambao kazi zao za sanaa au michezo zimeipatia sifa kubwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Historia inaonyesha kwamba Bikidude ni mwimbaji wa muziki wa taarabu toka visiwani Zanzibar. Anaangaliwa kama malkia wa muziki wa taarab na unyago hapa nchini ambaye kipaji chake kiligunduliwa na kuimarishwa na mkongwe wa muziki wa aina hiyo Siti binti Saad kati ya miaka ya 1880 mpaka 1950.

Bikidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, akiwa ni mtoto wa mfanyabiashara wa nazi enzi za ukoloni nchini Zanzibar.

Mpaka sasa haijafahamika tarehe ya kuzaliwa ya bibi huyo kwasababu sehemu kubwa ya historia zinazo husu historia ya maisha yake hazioani na hivyo kuwepo na taarifa ambazo ni za kubuni.

Mwaka 2005, Bikidude alipewa tuzo ya heshima ya dunia WOMEX tuzo ambazo zilibuniwa mwaka 1999 na mbazo wanazawadiwa watu ambao wamepata mafanikio makubwa katika muziki au wametoa mchango mkubwa katika muziki, umuhimu wa mtu katika jamii na hata , mafanikio ya kibiashara na kwa upande wake ilitokana na mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar.

Akiwa mdogo, Bikidude alisifiwa sana kutokana na sauti yake na katika miaka ya 1920 alianza kuimba na vikundi mbalimbali vya kiutamaduni.

Alipokuwa na umri wa miaka 13, baada ya kulazimishwa kuolewa aliamua kutoroaka na kuelekea Tanzania Bara.

Bikidude ni moja ya waimbaji wakongwe waliozunguka nchi zote za Afrika Mashariki akiimba taarab ambapo alitembelea miji mikubwa ya ukanda wa pwani pamoja na bara upande wa ziwa Victoria na Tanganyika.

Mwaka 1930, alirejea Dar es Salaam na kujiunga na kikundi cha Egyptian Taarab ambacho alidumu nacho kwa miaka mingi.

Katika miaka ya 1940 alirejea Zanzibar na kujenga nyumba yake iliyokuwa ya matope na kuanza maisha mapya hapo.

Alikuwa maarufu sana kwa shughuli za unyago ambazo ziliwaandaa masichana wadogo kuelekea katika ubalehe na kuingia katika maisha ya utu uzima.

Ni mtaalamu wa mambo hayo ya mila kongwe akifanya hivyo kwa wasichana akitumia mafunzo ya kitamaduni kuwaelekeza wasichana namna ya kuishi na waume zao na kuepuka migongano ya kifamilia na unyanyasaji wa mapenzi.

Sifa na jina la Bikidude lilikuwa na kusifika katika jamii yote ya Zanzibari na kuwa kielelezo cha utalii wa visiwa hivyo vya karafuu ambapo hoteli mbalimbali kubwa na zenye hadhi ya juu visiwani humo zimekuwa zikizipa majina migahawa ya hoteli jina la Bikidude, mfano 236 Hurumzi inatumia jina la mgahawa wake jina la 'Kidude'.

Moja ya nyimbo zake ambazo zilitamba na kumpatia umaarufu mkubwa mkongwe huyo ni Muhogo wa Jang'ombe ambao ulikamata kwenye mwambao wa Afrika Mashariki.
Bikidude ni hazina kubwa na mwalimu mzuri kwani inasemekana wasanii wengi wamepata mafunzo kutoka kwake.

Pamoja na umahiri wa msanii huyo lakini hajawahi kukumbwa na kashfa yoyote hadi sasa hivyo amekuwa na historia ya kipekee tofauti na wasanii wa sasa.

Wasanii wengine waliopewa nishani hiyo ni pamoja na kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo, kiongozi wa zamani wa bendi ya Dar es Salaam International, marehemu Marijani Rajabu, aliyekuwa msanii maarufu wa maigizo na filamu nchini, marehemu Fundi Saidi 'Mzee Kipara' na mwanariadha mkongwe, John Steven Akwari.

Gurumo, Bi Kidude na Akwari walihudhuria hafla hiyo ya kuvishwa nishani zao na Rais Kikwete wakati nishani za Marijani na Mzee Kipara zilipokelewa na watoto wao.

Bikidude hakuweza kwenda eneo la kupokea nishani kutokana na hali ya afya yake kutokuwa nzuri. Ilibidi Rais Kikwete amfuate mahali alipokuwa ameketi na kumtunukia nishani yake.

Bikidude, amedumu kwenye fani ya uimbaji kwa zaidi ya nusu karne na kwa sasa ni msanii pekee wa taarab mwenye sifa zilizotukuka kutokana na ukongwe wake na umahiri wake katika kuimba taarab.

Gurumo alianza muziki 1960 na kushiriki katika bendi mbalimbali kama vile Nuta, Juwata, Ottu, Atomic Jacc, Kiko Kids, Jamhuri Jazz, Kilwa Jazz, Rufiji Jazz, Mlimani Park, Msondo Ngoma.

Ametunga nyimbo nyingi zinazoelimisha jamii kuhusu kuheshimu na kufanyakazi kwa juhudi na maarifa, kulinda uhuru wa nchi, kudumisha usawa, haki na amani na kuwaasa wazazi kutimiza wajibu wao kwa kulea watoto na vijana kutimiza wajibu wao.

Marehemu Marijani, maarufu kama Jabali la Muziki, alifariki dunia mwaka 1995. Alitoa mchango mkubwa katika tasnia ya muziki, alishiriki kutunga na kurekodi nyimbo zaidi ya 103, ambazo zilirekodiwa RTD, nyimbo zake zilikuwa na mafunzo mengi kwa jamii na zinaendelea kupigwa katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Mzee Kipara mwaka 1962 alijiunga na waigizaji wa Redio Tanzania, pia ameshiriki maigizo na tamthilia nyingi za kwenye televisheni kama vile Hujafa hujaumbifa, Fukuto, Radi, Gharika, Tufani na Tetemo.

Mzee Akwari aliweka historia ya pekee nchini mwaka 1968 pale aliposhiriki mbio za marathoni za Olimpiki na kuumia goti na kutoka malengelenge, lakini aliushangaza ulimwengu alipoendelea na kumaliza mbio hizo. Alipoulizwa, alisema 'mimi sikutumwa kuja kuanza mbio, nimetumwa kumaliza mbio'. Maneno hayo yamekuwa yakitumika kama mifano duniani.


Sunday, January 6, 2013

JAHAZI KUJIVINJARI TRAVETINE USIKU WA LEO

 Big Daddy Mzee Yussuf.  Mkali wa taarab hapa nchini Mzee Yussuf leo amepania kukonga nyoyo za mashabiki wake katika show yake ya kwanza kuifanya tangu mwaka huu wa 2013 ulipoingia katika ukumbi wa Travetine Hoteli.

Nguli huyo ambaye natamba na wimbo unaokwenda hewani kwa jina la Wasiwasi wako atawaongoza waimbaji wengine wa kundi hilo kulishambulia jukwaa kuanzia saa tatu usiku mpaka riamba.

 Malkia Leila Rashid anaye atakuepo kwenye onyesho hilo bab kubwa kabisha tangu kuanza kwa mwaka huu.

 Mwasiti naye ataimba

 Mohammed Ali 'Mtoto Pori' ataimba kibao chake kipya kinachofahamika kama 'Kazi mnayo'

 Timu yote hii itakuepo na kila mmoja ataimba kwa raha zake kabisa hivyo mashabiki na wapenzui wote munatakiwa kuhudhuria onyesho hilo la aina yake.

 Mfalme Mzee Yussuf akiimba na wacheza kiduku wake
 Fatma Ali

 Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf.

 Rahma Machupa akitunzwa na shabiki wake.

 Mwasiti Kitoronto.

 Mzee Yussuf akiimba.

 Kutoka kushoto ni Leila Rashid, Fatma Kasimu na Kidawa.

 Wazee wa kazi wakiwa kwenye pozi ni Chid Boy na Amigo

 Hao ni Mwasiti na na Rahma Machupa

 Nogesha baba nogesha.

 Mashabiki wa Jahazi wakitibwirika

 Baba Warida Mussa Bezi
 Mzee Yussuf akicheza kidugu

 Warembo wa Jahazi wakiwa kazini
 Ni kiduku kwenda mbele tu
Mzee Yussuf akiimba kwa hisa.

Wakali wa taarabu hapa nchini Jahazi leo watafanya onyesho lao la kwanza tangu kuingia kwa mwaka huu katika ukumbi wao wa nyumbani wa Travetine Hoteli kuanzia saa tatu usiku mpaka riamba.

Kiongozi wa Jahazi Mzee Yussuf amesema onyesho hilo bab kubwa litatakuwa maalumu kwa wapenzi na mashabiki wao na kwamba wataimba nyimbo zao zote mpya na na zile zinazoendelea kuwika kwenye viunga mbalimbali vya burudani.

Amewaomba mashabiki na wapenzi wao kujitokeza kwa wingi ili kupata burudani ya kutosha na kuridhisha katika onyesho hilo.