Powered By Blogger

Tuesday, October 30, 2012

JAHAZI KUVAMIA KITUNDA

 Big Daddy Mzee Yussuf
 Mohammed Alli
 Fatma Ali
 Mauji anachana nyuzi
 Amigo
 Fatma Mcharuku
 Anaringa naringa
 Miriam Amour
 Mussa Bezi
 Malkia Leila Rashid
 Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf
 Mgeni Said
Waimbaji wa Jahazi

Jahazi usiku wa leo itaporomosha burudani ya kufa mtu kwa wakazi wa Kitunda na Vitongoji vyake.

Onyesho hilo litaanza saa tatu usiku na Jahazi itatumia muda huo kutambulisha albamu yao mpya itakayozinduliwa mwishoni mwa mwaka huu.

Mkurugenzi wa Jahazi Mzee Yussuf atawaongoza waimbaji wa kundi hilo katika burudani hiyo kabambe

Sunday, October 28, 2012

Njoo Jahazi Travetine Usiku huu ukutane na waimbaji hawa

 Umuone Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf
 Ukutane na Big Daddy Mzee Yussuf
 Uonane na Mussa Bezi
 Kikosi hicho kitakuepo
 Hata dada na kaka utawaona hivi hivi
 Mcharuko atawapagawisha mashabiki wake
 Mauji akichana nyuzi zake
 Mashabiki watulivu kama hawa utakutananao
 Amigo hakosi abadani
 Hata Malkia Leila Rashid atatia timu
 Shosti Fatma Ali utakutananaye
 Kama hujawahi kumuona Mgeni Said leo utamuona
 Bibie Miriamu Amour atakuepo
 Mtoto Pori ndani ya nyumba
 Utamuona Mwasiti Kitorontro
Mussa Mipango

Wakali wa mipasho hapa nchini Jahazi usiku huu watakonga nyoyo za mashabiki wao katika ukumbi wa Travetine hoteli Magomeni.

Onyesho hilo ikiwa ni mfululizo wa shangwe za sikukuu ya eid el hajj zitaanza kurindima majira ya saa tatu usiku mpka majogoo.

Kiongozi wa Jahazi 'Big Daddy' Mzee Yussuf atakuwa nahodha katika onyesho hilo na atawaongoza waimbaji wote wa kundi hilo mahiri hapa nchini.


Saturday, October 27, 2012

MAMBO YA EXTRA BONGO HAYO

 Lebo ya bendi hiyo
 Ali Choki akiimba
 Wacheza show wa bendi hiyo wakiwajibika
 Kazi mzuri jembe
 Wakionyesha machejo yao
 Raha kwenda mbele
Choki akitoa burudani

MNYAMA ALAMBA KONI ZA AZAMU

 LEBO YA SIMBA
 WACHEZAJI WA SIMBA WAKIFURAHIA MOJA YA GOLI LAO
 HATOKI MTU HAPA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba jana iliziyeyusha koni za Azam baada ya kuinga timu hiyo kwa 3-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Azamu ilikuwa ya mwanzo kupata goli baada ya mshabuliaji wake mahiri John Boko 'Adebayo' kuiadikia timu hiyo bao la kwanza.

Hata hivyo, Simba ilizinduka na kulishambulia lango la Azamu kama nyuki na ndipo mshambuliaji hatari wa Simba aliyetokea Azam, Mrisho Ngasa aliposawazisha goli hilo.

Emmanuel Okwi alizidisha machungu langoni mwa Azamu baada ya kupachika magoli mawili na hadi kipenga kinamalizika Simba tatu na Azamu moja.

Kwa matokeo hayo Simba iko kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 23 na kuwaacha nyumba mahasimu wao Yanga wakiwa na pointi 20 huku Azamu wakishika nafasi ya tatu.

Nao Yanga walifanikiwa kuharibu gwaride la JKT Olijoro baada ya kuwafunga goli moja kwa buyu katika mchezo uliopigwa mjini Arusha.

Bao la Yanga lilifungwa na Mbuyu Twite na hadi mwisho wa mchezo Yanga ilitoka uwanjani kifua mbele dhidi ya timu hiyo.

Sunday, October 21, 2012

NJOO TRAVE UKUTANE NA WAIMBAJI HAWA

 HADIJA YUSSUF
 UTAWAONA HAWA WOTE
 UMUONE MAUJI AKICHANA NYUZI
 UTAKUTANA NA MOHAMED ALI
 FATMA ALI
 UMUONE MZEE YUSSUF
 UTAKUTANA NA MASHABIKI WASTARAABU KAMA HAWA
 UTAMUONA AMIGO
 CHIDI BOY ATAKUEPO
 UKUTANE NA FATMA MAHAMOUD
 UONANE NA MALKIA LEILA RASHID
 MUSSA BEZI UTAKUTANANAYE
 MWASIRI KITORONTO UTAMUONA
UMUONE MUSSA MIPANGO