Powered By Blogger

Tuesday, May 29, 2012

WAIMBAJI NGULI WA KUNDI LA JAHAZI MWANNE OTHAMAN AKIWA NA FATMA MACHUPA

Waimbaji wanaochipukia kwa kasi katika kundi la mipasho la Jahazi Fatma Machupa (kushoto) akiwa na Mwanne Othaman kwenye onyesho la kundi hilo.

MZEE YUSSUF AKIJIACHIA KWA RAHA ZAKE

KIONGOZI WA KUNDI LA JAHAZI MFALME MZEE YUSSUF AKIPAGAWISHA JUKWAANI AKIWA NA PAMBA ALIZONUNUA NCHINI MAREKANI ZENYE THAMANI YA MAMILIONI YA SHILINGI.

KIONGOZI HUYO NA MUIMBAJI MAHIRI WA TAARAB HAPA NCHINI NA NJE YA NCHI AMEKUA MUIMBAJI PEKEE MWENYE KUPANGILIA PAMBA.

SAUTI YA CHIRIKU HADIJA YUSSUF AKITOA BURUDANI

FATMA KASIM AKITUMBUIZA JUKWAAANI

MFALME MZEE YUSSUF AKIKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE

Monday, May 28, 2012

KUNDI la muziki wa mwambao la Jahazi limeahidi kuendelea kutoa burudani yenye kiwango cha hali ya juu na imewashukuru wapenzi na mashabiki wake kwa kuliunga mkono kundfi hilo mahiri la taarab hapa nchini.

Ahadi hiyo imetolewa na mkurugenzi wa kundi hilo Mfalme Mzee Yussuf alipokuwa akizungumza na mwandishi wa blog hii jijini Dar es Salaam.

Mfalme alisema kundi hilo ambalo hivi sasa limejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kupiga burudani ya aina yake inayowasisimua wapenzi na mashabiki wao.

Alisema Jahazi itaendelea kuwapa raha wapenzi na mashabiki wao na kundi hilo litaendelea kuwapa raha kwa kuimba na kutunga nyimbo zinazoenda na wakati.

MZEE YUSSUF NA DADA YAKE