Powered By Blogger

Sunday, January 29, 2012

JAHAZI KUWASHA MOTO TRAVE LEO

WAKALI WA MUZIKI WA TAARAB NCHINI, JAHAZI MORDEN TAARAB LEO WATAPOROMOSOSHA BURUDANI YA NGUVU KATIKA UKUMBI WAO WA NYUMBANI ULIOPO TRAVETINE HOTEL, MAGOMENI DAR ES SALAAM.

KUNDI HILO LINALOTAMBA NA KIBAO CHAKE CHA MPENZI CHOKLETI, LINATARAJIA KUANZA BURUDANI SAA TATU USIKU HADI MAJOGOO.

KUNDI HILO LITASHUKA VIWANJANI NA WAIMBAJI WAKE MAHIRI AKIWEMO MALKIA LEILAH RASHID, FATMA MCHARUKO, MIRIAM AMOUR, FATMA ALLY. MOHAMED ALLY 'MTOTO PORI, ABUBAKAR SUDI 'AMIGO' FATMA KASIM NA WENGINE WENGI.

MKURUGENZI WA KUNDI HILO HAMIS BOHA ALISEMA ONYESHO HILO NI MAALUMU KWA WAPENZI NA MASHABIKI WAO WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA VITONGOJI VYAKE.