'Big Daddy' Mzee Yussuf leo kuandika historia nyingine kwenye tasnia ya taarab hapa nchini kwani muda mfupi ujao atazindua albamu yake ya tisa kwenye ukumbi wa travetine hoteli Magomeni.
Uzinduzi wa albamu hiyo iliyopewa jina la Wasiwasi wako utaanza saa mbili usiku ambapo Mfalme Mzee Yussuf na kundi lake litakapoingia katika uwanja huo kwa staili ya kipekee.
Mzee Yussuf amepania kufanya maajabu katika onyesho hilo na amewaahidi wapenzi na mashabiki wake kupata ladha na vitu tofauti katika usiku wa leo.
Amesema tiketi kwa ajili ya onyesho hilo kabambe zinapatikana mlangoni na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Malkia Leila Rashid naye ataimba wimbo mpya kabisa katika albamu hiyo.
Mohammed Ali naye ataimba usiku wa leo ni wimbo mpya kabisa
Fatma Ali ataimba wimbo wake mpya
Hadija Yussuf ataimba pia
Fatma Mahamoud
Sunday, December 30, 2012
Sunday, December 16, 2012
JAHAZI KUKAMU TRAVE USIKU HUU
Big Daddy Mzee Yussuf atatoa burudanmi maridhawa leo katika ukumbi wa Travetine Hoteli ambapo Jahazi itakonga nyoyo za mashabiki wake usiku huu
Mtoto wa Mfalme Amigo
Malkia Leila Rashid
Mtoto Pori Mohammed Ali
Ni shost Miriamu Amour anayetamba na wimbo katika bendi ya Jahazi
Unaweza kumwita Fatma Shobo muimbaji mahiri kabisa wa Jahazi
SaUTI YA Chiriku Hadija Yussuf akiwa na Director Mohamed Mauji. Hadija anatamba na wimbo usemao Zibeni njia sio riziki
Huyo ni Fatma Mcharuko au Mama Kijacho akimba ambapo hivi sasa anatamba na wimbo wake usemao Mtaniona hivi hivi
Fatma Kasimu akiwa na Mfalme Mzee Yussuf. Fatma anatamba na wimbo wake Hakuna Mkamilifu
Big Daddy akiimba na mashabiki wake.
Usiku wa leo Jahazi imedhamiria kutoa burudani ya aina yake katika ukumbi wa Travetine Hoteli uliopo Magomeni Dar es Salaam.
Onyesho hilo kamambe litaanza saa tatu usiku mpaka majogoo ambapo mashabiki wa bendi hiyo mahiri wataanza kununua tiketi za uzinduzi wa albamu ya 9 wa bendi hiyo utakaofanyika Desemba 31 mwaka huu, katika ukumbi Travetine Hoteli.
Mashabiki watakaonunua tiketi leo watauziwa kwa sh. 15000 badala ya sh. 20,000 siku ya uzinduzi.
Mkurugenzi wa Jahazi Mzee Yussuf alisema wameamua kuuza tiketi hizo mapema ili kutoa fursa kwa mashabiki wao kuzipata kabla ya siku ya uzinduzi huo.

Sunday, December 9, 2012
NJOO JAHAZI PALE TRAVE UKUTANE NA WAIMBAJI HAWA
Fatma Mahamuod 'Mcharuko'
Kipenzi cha mashabiki wengi Mfalme Mzee Yussuf
Umuone mtoto wa Mfalme Abubakari Sudi 'Amigo' na Full shangwe yake
Ukutane na Sauti ya Chiriku Hadija Yussuf akifanya mambo yake
Mwasiti Kitoronto atakuepo
Utamuona Malkia Leila Rashid bila ya chenga
Mtoto Pori Mohammed Ali ataimba
Shosti Fatma Ali atakuepo
Ukutane na Mussa Mipango mfalme wa Bass Tanzania
Mgeni Said atakuepo
Director Mohammed Mauji
Utamuona Big Daddy Mzee Yussuf
Utakutana na Miriamu Amour
Rahma Machupa
MABINGWA wa muziki wa mipasho nchini, Jahazai usiku huu utakonga nyoyo za mashabiki wake katika ukumbi wa Taravetine Hoteli Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Jahazi wakiongozwa na Mfalme Mzee Yussuf watatia nanga katika ukumbi huo kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo.
Bendi hiyo mahiri na iliyosheheni waimbaji makini watapiga nyimbo zao mpya na zile zinazotamba kwenye anga za burudani hapa nchini.
Mkurugenzi wa Jahazi, Big Daddy Mzee Yussuf alisema onyesho hilo watatumia katika kutambulisha nyimbo zao mpya ambazo watazizindua mwishoni mwa mwezi huu katika ukumbi huo.

RAIS KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 51 YA UHURU WA TANGANYIKA
Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete akiingia uwanja wa Uhuru tayari kwa maadhimisho hayo, amefuatana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange
Gwaride likipita mbele ya Amiri Jeshi
Amiri Jeshi, Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik akisalimiana na Rais wa Congo, Joseph Kabila
Viongozi mbalimbali waliohudhuria
Nia askari wa kikosi cha FFU wakipita kwa mwendo wa haraka
Kikosi cha bendera
Vijana wa Halaiki
Gwaride
Rais Kikwete akikagua gadi ya askari Magereza wanawake
AMIRI Jeshi Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete aliwaongoza maelfu ya Watanzania kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika.
Sherehe hizo zilifanyika kiatika uwanja wa Uhuru, Temeke Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.
Viongozi waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mzee Mwinyi, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, Mama Maria Nyerere, Mama Fatma Nyerere, mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu, wabunge, wawakilishi, mabalozi na marais kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Wananchi walifurika kwa wingi katika sherehe hizo ambapo uwanja wa Uhuru ulitapika na baadhi yao walilazimika kuhamia uwanja wa taifa.

Monday, December 3, 2012
Mfahamu Rahma Machupa kinda wa Jahazi Morden atayemvulia kofia Mfalme Mzee Yussuf
Rahma Machupa
Shostito Rahma akiimba
RAHMA Machupa ni muimbaji chipukizi wa taarab anayeibukia kwa kasi katika tasnia ya muziki huo hapa nchini.
Muimbaji huyo, anayetokea kwenye familia ya wanamuziki, katika siku za hivi karibuni ameonyesha uwezo mkubwa katika kundi lake la Jahazi Morden Taarab 'Wana wa nakshinakshi'.
Akizungumza na mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Rahma anasema kipaji chake cha uimbaji kilianza kuibuka akiwa katika shule ya sekondari ya Sinza.
Anasema akiwa katika shule hiyo alikuwa akishiriki kuimba nyimbo mbalimbali kwa kushirikiana na wanafunzi wenzake hususan wakati wa sherehe.
Rahma, anasema mwaka 2010 baada ya kuhitimu kidato cha nne katika shule hiyo alijiunga na kundi la Mashauzi Classic chini ya Isha Mashauzi 'Jike la Simba'.
Anasema baada ya kujinga na kundi hilo na kuonyesha uwezo mkubwa, alitunga wimbo unaofahamika kama 'Sijamuona kati yenu wa kunirusha roho'
Rahma anasema wimbo huo, ulikonga vilivyo nyoyo za wapenzi wa burudani na kuanzia hapo jina lake lilianza kusikika kila kona ya mtaa.
Anasema pamoja na kuachia kibao hicho, hakufanikiwa kukaa sana kwenye kundi hilo kutokana na sababu mbalimbali na ndipo alipojiunga na Jahazi.
Muimbaji huyo mwenye umbo la wastani na sauti maridhawa, anasema baada ya kujiunga na Jahazi chini ya 'Mfalme' Mzee Yussuf aliendelea kuonyesha uwezo wake wa uimbaji.
"Kwa kweli baada ya kujiunga na Jahazi kipaji changu kimezidi kukua na kadri siku zinavyokwenda nazidi kujipatia umaarufu kwa mashabiki wangu.
"Juhudi na uwezo mkubwa nilizozionyesha katikan kundi la Jahazi ndio zimemshawishi Mzee Yussuf kunipa wimbo katika albamu yetu mpya itakayozinduliwa hivi karibuni," anasema.
Anasema kutokana na uwezo na umahiri alionyesha akiwa na kundi hilo, amekabidhiwa wimbo unaofahamika kama Nipe stara na kudai utafanya vizuri kwenye anga za burudani.
Rahma anasema wimbo huo, ni miongoni mwa nyimbo zitakazokuwemo kwenye albamu mpya ya Jahazi itakayozinduliwa mwezi ujao.
"Najiamini naweza na nitafanya kila liwezekanavyo nifanye vizuri kwenye tasnia hii ya muziki wa mwambao ili nifikie lengo nililokusudia, ninawaahidi mashabiki wangu sitowaangusha," alijigamba muimbaji huyo.
Anasema akiwa katika kundi hilo atatumia uwezo wake wote kufikia lengo lake la kuwa muimbaji bora na mwenye uwezo mkubwa kama walivyo waimbaji wengine.
Rahma, anasema binafsi anavutiwa sana na muimbaji mkongwe wa taarab hapa nchini, Rukia Ramadhani kutokana na uimbaji wake na tungo zake maridhawa.
Anasema mbali na muimbaji huyo, anavutiwa na Hadija Yussuf na Leila Rashid na kwamba anatamani siku moja awe na uwezo kama waimba hao.
Akimzungumzia Mzee Yussuf, Rahma anasema ni muimbaji mahiri asiyependa makuu na hana upendeleo ndani ya kundi lake.
Anasema Yussuf, amekuwa na mchango mkubwa kwa waimbaji wake hususan chipukizi na kwamba anawafundisha mambo mengi ya muzi na maisha.
Rahma, anasema matarajio yake ni kumiliki kundi lake la muziki na kuwa muimbaji bora ndani na nje ya nchi.
Pamoja na kuwa muimbaji bora, anaelekeza nguvu zake kwenye elimu na kwamba anafikiria kurudi darasani kuendelea na masomo mpaka afike chuo kikuu.
Muimbaji huyo, anasema amezaliwa miaka 22 iliyopita jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kati ya wanane katika familia yao.

Jahazi kuachia albamu mpya mwishoni mwa mwezi huu
Mtoto wa Maflme Abubakari Sudi Amigo
Amigo akiringa na mashabiki wake
Mtoto pori huyoooooooooooo
Mzee wa gita huyo akifanya majambozi
Mashabiki kwa roho kwatu kabisa
Mambo ya Malkia hayo
Mzee Yussuf akiimba
Kiduku kama kawa
Mcharuko na mambo yake
Fatma Ali kwa raha zake
Oohh raha nazijua, huyo ni Mzee Yussuf akiimba
Husna Machupa
Miriam Amour akitoa burudani
Hadija Yusuf sauti ya Chiriku
Big Daddy akikumbushia enzi zake
Malkia akitoa burudani
Musa Mipango akikung'uta gita
Waimbaji wa Jahazi
Mtaalamu Chid Boy akipiga kinanda
Mashabiki wa Jahazi wakikonga nyoyo zao
Mfalme Mzee Yussuf akiimba na dada yake Hadija Yussuf
Fatma Mcharuko akiimba
Wazee wa kiduku
Mke wa Mfalme Malkia Leila Rashid
Mpapasa kinanda wa Jahazi, Mgeni Said
Mwasiti Kitoronto
Wakali wa muziki wa taarba hapa nchi wanendelea kufanya maonyesho yao kwa ajili ya kuitambulisha albamu yao mpya itakayozinduliwa mwishoni mwa mwaka huu.
Kundi hilo limekuwa likiitambulisha albamu hiyo kwenye kumbi tofauti jijini Dar es Salaam na mikoa jirani.
Albamu hiyo imesheheni nyimbo kali na itazinduliwa Desemba 31 mwaka huu, katika ukumbi wa Travetine Hoteli Magomeni.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Mzee Yussuf alisema uzinduzi wa albamu hiyo utakuwa wa aina yake kwani utasindikizwa na buradani kadhaa kutoka kwa wasani mbalimbali na makundi mengine ya muziki ambayo yatafahamika hapo baadae.
Jahazi inazindua albamu hiyo ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu ilipoachia albamu yake ya Mpenzi Chokleti ambayo inatamba kwenye viunga mbalimbali vya burudani hapa nchini.

Subscribe to:
Posts (Atom)